JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU Simu: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz ...
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425 |
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 10 Februari, 2017 amemteua Bw. Rogers William Sianga kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (Drug Control and Enforcement Authority).
Kamishna Mkuu Rogers William Sianga atasaidiwa na Bw. Mihayo Msikela ambaye anakuwa Kamishna wa Operesheni na Bw. Fredrick Kibuta ambaye anakuwa Kamishna wa Intelijensia.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Anna Peter Makakala kuwa Kamishna Mkuu wa Uhamiaji.
Kabla ya uteuzi huo Dkt. Anna Peter Makakala alikuwa Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji Moshi, kilichopo Mkoani Kilimanjaro.
Uteuzi huu unaanza mara moja na wateule wote wataapishwa Jumapili tarehe 12 Februari, 2017 saa 5:00 Asubuhi, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
10 Februari, 2017

COMMENTS