RAIS MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO TOKA KWA MABALOZI WA SAUDI ARABIA, MOROCCO, ZAMBIA, CUBA, IRAN NA BURUNDI LEO
HomeJamii

RAIS MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO TOKA KWA MABALOZI WA SAUDI ARABIA, MOROCCO, ZAMBIA, CUBA, IRAN NA BURUNDI LEO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU Simu: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz ...

WANAFUNZI 250 WAPATA MAFUNZO YA GIRL GUIDES TEMEKE
PROFESA NGOWI ATOA USHAURI KUHUSU UJENZI WA VIWANDA NCHINI TANZANIA
MATUKIO MBALIMBALI YA MAADHIMISHO YA SIKU YA KISUKARI DUNIANI - MNAZI MMOJA DSM

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULUDescription: Description: Description: Description: Description: Coat of Arms
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz               

Faksi: 255-22-2113425


OFISI YA RAIS,
     IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 08 Februari, 2017 amepokea hati za utambulisho za Mabalozi 6 kutoka nchi mbalimbali walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini.
Mabalozi wote wana makazi yao hapa Jijini Dar es Salaam na wamekabidhi hati zao za utambulisho kwa Mhe. Rais Magufuli Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mabalozi hao ni Balozi wa Ufalme wa Kiarabu wa Saudi Arabia Mhe. Mohamed Ben Mansour Al Malek, Balozi wa Ufalme wa Morocco Mhe. Abdelilah Benryane, Balozi wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Benson Keith Chali, Balozi wa Jamhuri ya Cuba Mhe. Lucas Domingo Hernandez Polledo, Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Mhe. Mousa Farhang na Balozi wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Gervais Abayeho.
Pamoja na kupokea hati zao za utambulisho Mhe. Rais Magufuli amewakaribisha Mabalozi hao hapa nchini na kuwahakikishia kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi zao katika nyanja mbalimbali hasa uchumi kwa manufaa ya pande zote.
“Mhe. Balozi najua kuwa Saudi Arabia imekuwa ikishirikiana na Tanzania kutekeleza miradi mingi ya ujenzi wa miundombinu na bado kuna miradi mingi tutashirikiana, naomba umfikishie salamu zangu nyingi Mhe. Mfalme wa Saudi Arabia kuwa tutaendelea kushirikiana” amesema Mhe. Rais Magufuli alipokuwa akizungumza na Mhe. Balozi Mohamed Ben Mansour Al Malek.
“Nitafurahi sana kuona Cuba inakuja kujenga viwanda vingi vya kuzalisha dawa hapa Tanzania, tunataka kuondokana na uagizaji wa dawa kutoka nje ya nchi ili kupunguza gharama kubwa ambazo Serikali inabeba kwa sasa kwa kuagiza dawa kutoka nje” Mhe. Rais Magufuli amemueleza Balozi wa Cuba hapa nchini Mhe. Lucas Domingo Hernandez Polledo.
Balozi wa Morocco hapa nchini Mhe. Abdelilah Benryane amemueleza Rais Magufuli kuwa pamoja na mambo mengine ambayo nchi hiyo inaendelea kushirikiana na Tanzania tayari imeanza mchakato wa kutekeleza ahadi ya Mfalme wa Morocco Mtukufu Mohammed VI ya kujenga uwanja wa mpira Mjini Dodoma.
Akizungumza na Balozi wa Zambia hapa nchini Mhe. Benson Keith Chali Mhe. Rais Magufuli amesema anatarajia ujio wake pamoja na mambo mengine utasaidia kuharakisha mchakato wa kuimarisha utendaji kazi na ufanisi wa reli ya TAZARA na bomba la mafuta la TAZAMA kwa manufaa ya nchi hizi mbili.
Kwa Balozi wa Burundi hapa nchini Mhe. Gervais Abayeho, Mhe. Rais Magufuli amemhakikishia kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi hiyo kama ndugu na marafiki wa kihistoria na kwamba anaamini kuwa juhudi zinazoendelea kufanywa na Mpatanishi wa Mgogoro wa kisiasa nchini humo Mhe. Benjamin William Mkapa ambaye ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu nchini Tanzania zitazaa matunda.
Mabalozi wote wamempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa hatua anazochukua kujenga uchumi wa Tanzania, kukabiliana na rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na kusimamia uwajibikaji wa viongozi na watumishi wa umma.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
08 Februari, 2017

 Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea hati za utambulisho toka kwa Balozi wa Saudi Arabia nchini Mhe. Mohamed Ben Mansour Al Malek Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jumatano Fenruari 8, 2017.
 Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea hati za utambulisho toka kwa Balozi wa Morocco Mhe Abdellah Benryane Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jumatano Fenruari 8, 2017.
  Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea hati za utambulisho toka kwa Balozi wa Zambia Mhe. Benson Keith Chali  Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jumatano Fenruari 8, 2017. 
 Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea hati za utambulisho toka kwa Balozi wa Cuba Mhe. Lucas Dominingo Hermandes Polledo  Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Fenruari 8, 2017.
 Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea hati za utambulisho toka kwa Balozi wa Iran Mhe Mousa Farhang  Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jumatano Fenruari 8, 2017.
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea hati za utambulisho toka kwa Balozi wa  Burundi  nchini Mhe. Gervais Abayeho Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jumatano Fenruari 8, 2017. (PICHA NA IKULU)
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RAIS MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO TOKA KWA MABALOZI WA SAUDI ARABIA, MOROCCO, ZAMBIA, CUBA, IRAN NA BURUNDI LEO
RAIS MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO TOKA KWA MABALOZI WA SAUDI ARABIA, MOROCCO, ZAMBIA, CUBA, IRAN NA BURUNDI LEO
https://lh6.googleusercontent.com/vY_My_Z_14iRMhvtUNZH5e9rUrEbZxp-jTlbmhRkYq_74ulDWFOXXNaZ3rQaeUSNXD2aTsmO7yCP3GCttdIxy9JjXjzSM5nK9dzX8Wacy17z3KeXDicfb60qS_1N4CTdIRkbUSinSMFpVk3CBA
https://lh6.googleusercontent.com/vY_My_Z_14iRMhvtUNZH5e9rUrEbZxp-jTlbmhRkYq_74ulDWFOXXNaZ3rQaeUSNXD2aTsmO7yCP3GCttdIxy9JjXjzSM5nK9dzX8Wacy17z3KeXDicfb60qS_1N4CTdIRkbUSinSMFpVk3CBA=s72-c
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/02/rais-magufuli-apokea-hati-za.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/02/rais-magufuli-apokea-hati-za.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy