Na Georgina Misama – MAELEZO. Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limejipanga kumaliza kero ya makazi ya nyumba kwa watanzania ifik...
Na Georgina Misama – MAELEZO.
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limejipanga kumaliza kero ya makazi ya nyumba kwa watanzania ifikapo mwaka 2025.
Hayo
yamesemwa na Meneja Mauzo wa Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) Bw.
Erasto Chilambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo
Jijini Dar es Salaam.
Ili
kutimiza azma hiyo,Chilambo alibainisha kuwa nyumba zisizopungua elfu
30 zitajengwa kwa ajili ya kuuzwa na kupangishwa ambapo katika nyumba
hizo watu wa kipato cha chini, kati na juu ndio walengwa.
“Katika
mkakati huu, Shirika limekusudia kujenga nyumba 12000 kwa ajili ya watu
wa kipato cha chini, nyumba 13500 kwa ajili ya watu wenye kipato cha
kati na nyumba 2700 kwa ajili ya watu wenye kipato cha juu.” Alisema
Chilambo.
Aidha,
Shirika linajenga majengo 1800 ya kibiashara katika maeneo mbalimbali
nchini, ambayo yanatazamiwa kukamilika ifikapo 2025.
“Katika
kuunga mkono uamuzi wa serikali wa kuhamia Dodoma, shirika linajenga
nyumba za makazi 300 zitakazouzwa kwa watumishi wa Serikali, ambazo zina
ukubwa tofauti zenye vyumba 3 kila moja.” Alisema Bwn.Charahani.
Tangu
kuanzishwa kwake Shirik la Nyumba limekuwa likimiliki na kuuza majengo
mbalimbali. Hivi sasa shirika linamiliki MAJENGO 2483 yenye sehemu 18121
za makazi na biashara katika Mikoa ya Tanzania Bara.
Meneja
Mauzo wa Shirika la Taifa la Nyumba (NHC) Bw. Erasto Chilambo
akizungumza na waandishi wa Habari Leo Jijini Dar es salaam kuhusu
mkakati wa shirika hilo kujenga nyumba 300 zitakazouzwa kwa watumishi wa
umma Mkoani Dodoma ili kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa
makazi kwa watumishi wanaohamia Mkoani humo na kuunga mkono juhudi za
Serikali kuhamia mkoani humo.kushoto ni Afisa Habari wa Shirika hilo Bi
Edith Nguruwe.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa NHC leo Jijini Dar es Salaam.
COMMENTS