Msanii wa Filamu na Muigizaji mahiri hapa nchini Steve Nyerere, akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar kuhusiana n...
Msanii
wa Filamu na Muigizaji mahiri hapa nchini Steve Nyerere, akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar kuhusiana na mambo
mbalimbali yaliyotokea hivi karibuni, likiwemo suala la ujumbe wa sauti
ambao umekuwa ukisambazwa katika mitandano ya kijamii ukimuhusisha yeye
Steve pamoja na Mama Wema Sepetu.
''Kulikuwa
na maongezi ya simu kati ya mimi na mama Sepetu, mimi ndio nilikuwa
naogea na mama Sepetu, Maneno yasipindishwe",amesema Steve Nyerere na
kuongeza kuwa yeye ana miaka 25 kwenye sanaa, inakuaje leo mtu anatoa
ama anasambaza mambo binafsi waliokuwa wakiyazungumza kwa ajili ya
kumsadia mtoto wake.
Msanii
wa Filamu nchini, Steve Nyerere, leo amekutana na waandishi wa Habari,
ambapo katika mkutano huo amekanusha kuwa Wasanii nchini hawakidai Chama
Cha Mapinduzi fedha kwa ajili ya Mradi wa Mama Ongea na Mwanao, wakati
wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Katika
Mkutano huo STEVE NYERERE amesisitiza kuwa kilichosemwa na WEMA SEPETU
kuwa anaidai CCM fedha ni uongo, kwani walilipwa huku akisema Msanii
aliyelipwa fedha nyingi katika kazi hiyo ni Wema Sepetu, hivyo
anashangaa kusikia akidai kuwa hajalipwa.
Mradi
wa Mama Ongea na Mwanao uliratibiwa na Steven Nyerere huku akisaidiwa na
Wema Sepetu na kazi yake ilikuwa ni kutoa elimu kwa wazazi kuwa karibu
zaidi na vijana wao wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Hata
Hivyo, Steve Nyerere, ametumia mkutano huo kukiri kuwa Sauti iliyotumwa
kwenye Mitandao ya Kijamii inayohusisha mazungumzo yake na Mama yake
Wema Sepetu ni ya kwake, hivyo amewaomba radhi viongozi wote aliowataja
katika mazungumzo hayo.
'Kulikuwa
na maongezi ya simu kati ya mimi na mama Sepetu, mimi ndio nilikuwa
naogea na mama Sepetu yasipindishwe,"Ile Sauti imekuja kuachiwa juzi
wakati watu wanahama chama, kwanini nirekodiwe? naamini wamefanya hivyo
makusudi", alisema Steve Nyerere
"Namuomba
radhi Rais Magufuli na Chama changu cha CCM, yanaongelewa mengi
ninayasikia, naomba radhi familia pia, niliteleza, nimetaja viongozi
katika ile sauti halafu mtu anakuja kuisambaza nimetaja viongozi wa
Nchi, Mama alichofanya amenikosea sana, lakini namuachia Mungu"alimaliza
kusema.
COMMENTS