Na Anthony John, Globu ya Jamii Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limesema Jalada la kesi ya kukutwa na bangi Ms...
Na Anthony John, Globu ya Jamii
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limesema Jalada la kesi ya
kukutwa na bangi Msanii maarufu na Mlimbwende , Wema Sepetu bado
linapitiwa na Mwanasheria wa Serikali na baada ya kukamilika kwa
upelelezi atapelekwa mahakamani.
Akizungumza
na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es
Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi Simon Sirro amesema jeshi la polisi
limeshafanya kazi yake hivyo taratibu za kisheria za kesi ya Msanii
huyo zinaandaliwa kwa ajili ya kumfikisha mahakamani.
Amesema
katika mapambano ya dawa kulevya, wananchi na raia wema wameaswa kuacha
kutoa habari za uvunjifu wa amani katika mkoa wa Dar es salaam,badala
yake wajikite kutoa taarifa zilizokuwa za kweli.
"Unapotoa
taarifa ambazo si za kweli haumdanganyi kamishina Sirro, unakuwa
unalidanganya Jeshi la polisi ,kwa ujumla naomba raia wema waendelee
kutoa taarifa lakini watoe taarifa za uhakika"amesema Sirro.
Pia
Siro ameongeza kuwa Jeshi la polisi limejipanga vizuri kwa kuwapokea
watakao fika siku ya ijumaa lakini kikubwa wafike waje waripoti.
COMMENTS