HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE YATENGA KATA 10 KWA AJILI YA KILIMO CHA MKATABA
HomeJamii

HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE YATENGA KATA 10 KWA AJILI YA KILIMO CHA MKATABA

Mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi wa kilimo cha mkataba kupitia Taasisi ya  Winamwanga Cultural Heritage Association  kwa niaba ya...

MWILI WA MKURUGENZI MKUU HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI MSTAAFU KUZIKWA LEO MAKABURI YA KINONDONI DAR ES SALAAM
BOHARI YA DAWA (MSD) YAWAHAKIKISHIA WAWEKEZAJI FURSA NCHINI
SERIKALI YAZINDUA USAMBAZAJI WA VIFAA VYA HOSPITALI NCHINI





Mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi wa kilimo cha mkataba kupitia Taasisi ya Winamwanga Cultural Heritage Association kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, ambaye ni Ofisa Maendeleo ya Jamii, Wanchoke Chinchibera akihutubia wadau wa kilimo wa wilaya hiyo wakati wa semina ya siku moja iliyohusu kilimo cha mkataba iliyofanyika juzi wilayani humo. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa mradi huo, Mwajuma Motto, Ofisa Kilimo na Umwagiliaji wa wilaya hiyo, Elliot Mwasabwite na Mwenyekiti wa Bodi wa Taasisi hiyo, Esabela Luoga. 



Semina ikiendelea.
Meza kuu.
Mmoja wa maofisa wa Taasisi hiyo, Wilson Kibugu akitoa maelezo kwa wadau wa kilimo wa wilaya hiyo wakati wa semina hiyo ya siku moja iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Wilaya hiyo.
Ofisa Utawala wa Taasisi hiyo, Fatma Shaib (kushoto), 
akisoma lisala.
Mgeni rasmi Wanchoke Chinchibera akipokea lisala kutoka kwa Ofisa Utawala wa Taasisi hiyo, Fatma Shaib.
Mratibu Mradi wa Kilimo wa Taasisi ya  Winamwnga Cultural Heritage Association, Saidi Simkonda (katikati), akitoa mada katika uzinduzi  wa mafunzo ya kilimo hai na mafunzo ya ufugaji wa kuku chotara na mafunzo ya utunzaji wa mazingira yaliyofanyika wilayani Kisarawe mkoani Pwani juzi. 
Ofisa Mauzo wa Kampuni ya Syngeta Tanzania Limited, John Ngoma akielezea ubora wa mbegu aina ya Sy 514 inayosambazwa na kampuni hiyo kupitia miradi ya kilimo ya taasisi hiyo.
Mkurugenzi wa Mradi wa kilimo wa Taasisi ya  Winamwnga Cultural Heritage Association, Mwajuma Motto (katikati), akizungumza katika uzinduzi wa mafunzo ya kilimo hai na mafunzo ya ufugaji wa kuku chotara na mafunzo ya utunzaji wa mazingira kwa kutumia vikundi vya ufugaji wa nyuki yaliyofanyika wilayani Kisarawe mkoani Pwani jana. Kulia ni Mwezeshaji, Filbert Luoga na kushoto ni mratibu wa miradi wa taasisi hiyo, Saidi Simkonda. 
Ofisa Kilimo na Umwagiliaji wa wilaya hiyo, Elliot Mwasabwite akichangia jambo kwenye semina hiyo.

 Dotto Mwaibale, Kisarawe

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani imetenga Kata 10 kwa ajili ya kilimo cha mkataba kitakachoendeshwa na Taasisi ya  Winamwanga Cultural Heritage Association.

Mratibu wa mradi huo kutoka taasisi hiyo, Saidi Simkonda akizungumza juzi katika uzinduzi wa mafunzo ya kilimo hai na mafunzo ya ufugaji wa kuku chotara na mafunzo ya utunzaji wa mazingira kwa kutumia vikundi vya ufugaji wa nyuki yaliyofanyika wilayani humo juzi alisema mradi huo umelenga kuwainua kiuchumi wananchi wa Kisarawe na Mkoa wa Pwani kiujumla.


Alisema taasisi hiyo imepanga kuanzisha vikundi vya kuweka na kukopa ili kuinua uchumi wa wananchi kupitia vikundi vya ujasiriamali wa kilimo hai na ufugaji wa kuku chotara pamoja na kuwawezesha kupata fursa za mikopo katika asasi za kifedha zilizopo wilayani humo.

"Taasisi yetu imejipanga kuanzisha kilimo cha mkataba ambapo mazao yatakayopatikana itayanunua na tayari serikali ya Kijiji cha Kuluwi imetoa ghala la kuhifadhia mazao hayo.

Mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo ambaye ni Ofisa Maendeleo ya Jamii, Wanchoke Chinchibera alisema mradi huo utawasaidia wananchi na kuwa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe imetenga kata kadhaa kwa ajili ya mradi huo ambazo ni Maluwi, Vikumburu, Kuluwi na Mafizi.

Alisema kwa sababu mradi huo ni mpya katika wilaya yao na utafanya shughuli zake kwa kilimo cha mkataba aliishauri taasisi hiyo kujenga ushirikiano mkubwa na wananchi kupitia vikundi ambavyo tayari vimesajili na majina yake kuwepo katika daftari ofisini kwa mkurugenzi wa halmshauri hiyo.

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE YATENGA KATA 10 KWA AJILI YA KILIMO CHA MKATABA
HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE YATENGA KATA 10 KWA AJILI YA KILIMO CHA MKATABA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhC-8cQ0iW60y283wQL-s1tZYE9WwQaF6vsHbiw4zp9t56T_7d5YkWdZGRExdQFG4kE8Wj7qpKLIfflDK02MBqclNtDSGRfYZjQ8UVoVfRVuL6xd7VEm0RAtTPvgqi226_MzSlg8Xac_uWW/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhC-8cQ0iW60y283wQL-s1tZYE9WwQaF6vsHbiw4zp9t56T_7d5YkWdZGRExdQFG4kE8Wj7qpKLIfflDK02MBqclNtDSGRfYZjQ8UVoVfRVuL6xd7VEm0RAtTPvgqi226_MzSlg8Xac_uWW/s72-c/1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/02/halmashauri-ya-wilaya-ya-kisarawe.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/02/halmashauri-ya-wilaya-ya-kisarawe.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy