Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo, Mjini Dodoma limepisha Muswada wa Sheria...
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo, Mjini Dodoma limepisha
Muswada wa Sheria ya Huduma ya Msaada wa Kisheria wa Mwaka 2016 (The
Legal Aid Bill, 2016).
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe alipokuwa
akitoa taarifa wakati wa kuwasilisha muswada huo amesema kuwa muswada
huo wa sheria umepitia hatua nyingi na umechukua muda mrefu hadi kufikia
hatua ya kujadiliwa na Bunge tukufu.
Aliendelea kwa kusema kuwa muswada huo unapendekeza kutungwa kwa sheria
ya msaada wa kisheria kwa lengo la kuanzisha (kwa mara ya kwanza katika
histori ya nchi) mfumo wa kisheria wa kusimamia, kuratibu, kurasimisha
na kutambua utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria katika mashauri yote
ya Jinai na Madai kwa mahitaji.
Aidha utaratibu uliokuwepo kwa miaka mingi kwa upande wa Serikali
unahusu baadhi tu ya makosa ya Jina, makosa yenye adhabu kubwa kama vile
ya kunyongwa hadi kufa na vifungo virefu. Ambapo huduma hiyo imekuwa
ikitolewa katika ngazi ya Mahakama Kuu pekee na kwa wigo mdogo tu pale
inapohitajika kwa maslahi ya haki na kwa maelekezo ya Jaji Mkuu au
yeyote aliyekasimiwa mamlaka ya kutoa maelekezo hayo.
“Kumekuwepo na ongezeko kubwa la mahitaji ya huduma ya msaada wa
kisheria na wasaidizi wa kisheria. Kutokana na hali hiyo, Serikali
imeona ulazima wa kuanzisha mfumo wa kusimamia na kuratibu utoaji wa
huduma hiyo ili kuhakikisha inatolewa na watu wenye sifa, kwa wahitaji
halisi na kwa taratibu zinazofahamika ili iendane na matakwa ya
kikatiba,” alifafanua Dkt. Mwakyembe.
Vile vile ameeleza kuwa muswada huo unalenga kuwatambua wasaidizi wa
kisheria, kufuta sheria ya msaada wa kisheria (katika mashauri ya
Jinai).
Kwa upande wake Mbunge Selemani Zedi amesema kuwa, muswada huo
utawasaidia wananchi ambao hawana uwezo wa kuwalipa Mawakili
wanapohitaji msaada wa Kisheria.
Aidha, Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson ameipongeza Serikali kwa muswada
huo muhimu ambao Bunge umeipitisha unasuobiria kutiwa saini na Mhe. Rais
ili kuwa Sheria.


COMMENTS