BREAKING NEWZ: RAIS MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA UJENZI WA TERMINAL III UWANJA WA NDEGE WA JULIUS NYERERE JIJINI DAR JIONI HII

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU Simu: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz ...


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULUDescription: Description: Description: Description: Description: Coat of Arms
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz               

Faksi: 255-22-2113425


OFISI YA RAIS,
     IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 08 Februari, 2017 amefanya ziara ya kushtukiza katika mradi wa ujenzi wa jengo jipya la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam (Terminal 3) na kuagiza shughuli za ujenzi wa uwanja huo ziendelee kuanzia kesho.
Awali Mkandarasi anayejenga uwanja huo ambaye ni kampuni ya BAM International alitangaza kusitisha ujenzi kuanzia leo kutokana na kutolipwa madai yake na Mhe. Rais Magufuli ameahidi kulipa fedha hizo haraka.
Hata hivyo, Mhe. Rais Magufuli ameelezea kusikitishwa kwake na namna mradi huo unavyotekelezwa ikiwemo Serikali kukubali gharama kubwa za mradi ambazo ni Shilingi Bilioni 560 kiwango ambacho ni kikubwa ikilinganishwa na jengo linalojengwa.
“Hivi kulikuwa na sababu gani za nyinyi wataalamu wa Serikali kukubali gharama kubwa namna hii, hivi hili jengo linafanana na Bilioni 560?
“Halafu mlikuwa na haraka gani kuidhinisha kuanza awamu ya pili ya ujenzi kabla ya kumaliza awamu ya kwanza?” amehoji Mhe. Rais Magufuli alipokuwa akiwauliza Wahandisi wa Wizara ya Ujenzi wanaosimamia ujenzi huo.
Kufuatia hali hiyo, Mhe. Rais Magufuli amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa Mnyaa aliyeongozana nae kuunda timu ya wataalamu watakaofanya tathimini ya utekelezaji wa mradi huo ikiwa ni pamoja na kuzungumza na Mkandarasi anayejenga uwanja huo na Mhandisi Mshauri ambao wamekubali kupunguza gharama za ujenzi wa mradi huo.
“Serikali italipa fedha ambazo Wakandarasi wanadai lakini, nataka Waziri uunde timu ya kufanya tathmini upya, ni lazima hii gharama ipungue, hatuwezi kumaliza fedha zote hizi wakati jengo halifanani na thamani hiyo” amesisitiza Dkt. Magufuli.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli ambaye ameonesha kutofurahishwa na dosari zilizoanza kujitokeza katika baadhi ya maeneo ya jengo hilo, amemuagiza Mhe. Waziri Mbarawa kuunda upya timu ya Wahandisi watakaosimamia mradi huo na ambao watafanya kazi kwa uzalendo na kusimamia ubora.
Kabla ya kuondoka uwanjani hapo Mhe. Rais Magufuli amekutana na wafanyakazi walioajiriwa katika shughuli za ujenzi wa uwanja huo na kuwahakikishia kuwa Serikali imechukua za kuhakikisha mradi huo unaendelea na kwamba kuanzia kesho wataendelea na kazi kama kawaida.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemsimamisha kazi Kaimu Katibu wa Tume ya Mipango (Wizara ya Fedha) Bi. Frolence Mwanri aliyeidhinisha kuanza kwa awamu ya pili ya ujenzi wa jengo hilo jipya la Uwanja wa Ndege kabla ya kumalizika kwa awamu ya kwanza ili kupisha uchunguzi.
Mhe. Dkt. Magufuli ameviagiza vyombo vinavyohusika kufanya uchunguzi katika mradi huo.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
08 Februari, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya kustukiza katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa Terminal III kuona maendeleo ya ujenzi unaondelea leo Jumatano February 8, 2017.(PICHA NA IKULU)



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  katika picha ya pamoja na baadhi ya wahandisi na makadrasai alipofanya ziara ya kustukiza katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa Terminal III kuona maendeleo ya ujenzi unaondelea leo Jumatano February 8, 2017




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya kustukiza katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa Terminal III kuona maendeleo ya ujenzi unaondelea leo Jumatano February 8, 2017

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: BREAKING NEWZ: RAIS MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA UJENZI WA TERMINAL III UWANJA WA NDEGE WA JULIUS NYERERE JIJINI DAR JIONI HII
BREAKING NEWZ: RAIS MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA UJENZI WA TERMINAL III UWANJA WA NDEGE WA JULIUS NYERERE JIJINI DAR JIONI HII
https://lh3.googleusercontent.com/lj6WOmZ9R6bgRQ11WpD7_0ui6ZKN3IbqpqHxLqN8iGRXLQmrvpHpuxl4kGi2fyAWvumFat7-hdsjDzPzvq7rtMdW_vk2rQtDmkoSvy7B9p_jKbYINpp3i6_3zrYEgO59q5kIk9tjXG8-NP6q3g
https://lh3.googleusercontent.com/lj6WOmZ9R6bgRQ11WpD7_0ui6ZKN3IbqpqHxLqN8iGRXLQmrvpHpuxl4kGi2fyAWvumFat7-hdsjDzPzvq7rtMdW_vk2rQtDmkoSvy7B9p_jKbYINpp3i6_3zrYEgO59q5kIk9tjXG8-NP6q3g=s72-c
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/02/breaking-newz-rais-magufuli-afanya.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/02/breaking-newz-rais-magufuli-afanya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy