Kwa miaka 9 mfululizo, Toyota Tanzania Ltd imekuwa mdhamini mkubwa wa Rotary Dar Marathon. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Ponya Uhai boresha J...
Kwa miaka 9 mfululizo, Toyota Tanzania Ltd imekuwa mdhamini mkubwa wa Rotary Dar Marathon. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Ponya Uhai boresha Jamii”, ambapo Toyota Tanzania kwa ushirikiano na Bank M mdhamini Mkuu wa Marathon ya mwaka huu watajumuika pamoja kufanikisha hafla hiyo.
Fedha zilizochangishwa mwaka huu, zimeelekezwa katika ujenzi wa klinik ya hospitali ya CCBRT ili kuboresha huduma za wagonjwa na upatikanaji wa ophthalmology, tiba ya kimwili na mazoezi. Huduma za Kliniki zitawafikia wagonjwa wenye ulemavu katika Hospitali ya CCBRT, kwa gharama nafuu
Mbio za mwaka huu zitajumuisha marathon kamili Kilomita 42.2, nusu marathon kilomita 21.2, mbio za baiskeli za Kilomita 42.2 na 21.2 pia matembezi ya kifamilia ya Kilomita 5 ambazo, zitaanzia viwanja vya The Green na kumalizika katika viwanja hivyo hivyo Msasani jijini Dar es Salaam. Wanariadha, watembeaji na waendesha baiskeli zaidi ya 15,000 wanatarajiwa kushiriki ambapo mlezi wa mbio hizo, Mheshimiwa, Rais mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Al Haji Ali Hassan Mwinyi, pamoja na wakimbiaji kutoka la Jeshi la Polisi Tanzania, Kenya, Uganda , Rwanda na Ethiopia pia watashiriki.
Toyota Tanzania kwa mara ya kwanza ilitambulishaa bidhaa zake nchini kwa Familia ya Karimjee Jivanjee kupitia International Motor Mart mwaka 1965. Mwaka 2015 Toyota Tanzania iliadhimisha miaka 50 ya kuwa msambazaji pekee mwenye hati pekee ya kusambaza bidhaa za Toyota.
Familia ya Karimjee Jivanjee inayo historia ndefu na imara katika Afrika Mashariki tangu mwaka 1825 ambapo familia hiyo kama wafanyabiashara walitokea nchini India, na kufikia kisiwa cha Zanzibar. Ambayo ilikuwa ni sehemu ndiyo ya biashara ilikuwa ikikuwa na kusawi ambapo kwa mwaka walikuwa wanaweza kufanya safari kati ya India na Afrika ya Mashariki na kuweza kuwa kundi linaloheshimika sana. Mwaka huu 2017 Karimjee Jivanjee Group ilisherehekea maadhimisha miaka yake 192, wamejijengea heshima ambayo mpaka sasa uhaminifu, uhadilifu na uwaminifu katika tasinia ya Ujasiliamali na uvumilivu, karama na wema.
Kwa vizazi saba, Familia ya Karimjee Jivanjee imejijengea heshima kubwa kwa msaada wa vitu mbali mbali kama vile kujenga shule na hospitali, kutoa udhamini wa masomo ya elimu ya juu (sayansi na technolojia), kutoa misaada ya kijamii na kuhamasisha uhifadhi wa wanyamapori. Taasisi ya Karimjee Jivanjee ni gari la msingi la Familia la kazi za kujitolea.
COMMENTS