WIZARA YA MAMBO YA NJE YAFAFANUA KUHUSU MKUTANO WA TUME YA PAMOJA NA USHIRIKIANO KATI YA TZ NA MALAWI
HomeJamii

WIZARA YA MAMBO YA NJE YAFAFANUA KUHUSU MKUTANO WA TUME YA PAMOJA NA USHIRIKIANO KATI YA TZ NA MALAWI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI Simu: 255-22-2114615, 211906-12 Barua pep...

HIVI UNAJUA KWAMBA SIMU YAKO INAWEZA KUKUPUNGUZIA UFANISI KAZINI?
WEEKLY BULLETIN, ISSUE NO.165
SERIKALI YAIPONGEZA BoT KWA KUELIMISHA WAANDISHI WA HABARI
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

Coat of Arms
Simu: 255-22-2114615, 211906-12
Barua pepe: nje@nje.go.tz
Barua pepe: gcu@nje.go.tz

Nukushi: 255-22-2116600

              

               20 KIVUKONI FRONT,
                          P.O. BOX 9000,
                 11466 DAR ES SALAAM,  
                                   Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Taarifa ya ufafanuzi kuhusu Mkutano wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Malawi
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ilikutana na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Januari, 2017 kwa ajili ya kutoa taarifa kwa umma kuhusu Mkutano wa Nne wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPCC) kati ya Tanzania na Malawi ambao umepangwa kufanyika mjini Lilongwe, Malawi tarehe 03 hadi 05 Febuari 2017.
Hata hivyo, vyombo vingi vya habari hususan Magazeti ya tarehe 27 Januari, 2017 vimeandika kwamba Mkutano huo ni maalum kwa ajili ya kujadili mgogoro wa Mpaka kati ya Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa pamoja na kesi ya Watanzania nane waliokamatwa kwa madai ya kuingia nchini Malawi bila kibali.
Wizara inapenda kuchukua nafasi hii kutoa ufafanuzi kwamba, suala la mgogoro wa mpaka limekwishatolewa taarifa na Wizara hivi karibuni kwamba lipo chini ya Jopo la Usuluhishi linaloundwa na Viongozi Wastaafu wa Afrika kutoka nchi za Ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo  Kusini mwa Afrika (SADC). Jopo hilo linaongozwa na Mhe. Joachim Chissano, Rais Mstaafu wa Msumbiji akisaidiwa na Mhe. Festus Mogae, Rais Mstaafu wa Botswana na Mhe. Thabo Mbeki, Rais Mstaafu wa Afrika Kusini.
Aidha, kuhusu suala la Watanzania nane waliokamatwa kwa madai ya kuingia nchini Malawi bila kibali lipo Mahakamani hivyo halitakuwa sehemu ya mazungumzo ya Mkutano wa Tume ya Pamoja.
Pia, Wizara inapenda kuujulisha umma kuwa licha ya kuwepo kwa mgogoro wa mpaka wa Tanzania na Malawi katika Ziwa Nyasa, mahusiano ya nchi hizi mbili yamezidi kuimarika siku hadi siku katika nyanja zote za kiuchumi, kisiasa na kijamii. Hata wananchi wa pande zote mbili za Ziwa wameendelea kuishi kwa amani na ushirikiano wa karibu.
Kwa mantiki hiyo,  Mkutano wa Nne wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati  Tanzania na Malawi ni njia mojawapo ya kuendelea kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizi mbili. Mkutano huu ambao ni wa kawaida, una lengo la kujadili na kutathmini hatua zilizofikiwa katika utekelezwaji wa makubaliano yaliyofikiwa katika Mkutano wa Tatu wa JPCC uliofanyika Tanzania, tarehe 24 hadi 30 Juni, 2003.
Aidha, mkutano huu utawaleta pamoja watalaam wa nchi hizi mbili kutoka Sekta mbalimbali kwa lengo la kujadili changamoto za ushirikiano katika sekta hizo, kubaini maeneo mapya ya ushirikiano pamoja na kuweka mikakati ya kutekeleza miradi ya pamoja itakayokubaliwa baina ya pande hizi mbili. Masuala mbalimbali ya  ushirikiano  yatakayojadiliwa kwenye mkutano huu yatahusu sekta za biashara na uwekezaji, usafirishaji, fedha, nishati, utalii, ulinzi na usalama uhamiaji, uvuvi na ardhi.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam, 27 Januari, 2017

 

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WIZARA YA MAMBO YA NJE YAFAFANUA KUHUSU MKUTANO WA TUME YA PAMOJA NA USHIRIKIANO KATI YA TZ NA MALAWI
WIZARA YA MAMBO YA NJE YAFAFANUA KUHUSU MKUTANO WA TUME YA PAMOJA NA USHIRIKIANO KATI YA TZ NA MALAWI
https://lh3.googleusercontent.com/0fQEstwagC-PABXvrGd5iWZsYwn8HQD4uqiS1YW3GrStq2FHUz98Uq0Tucw8rfKrhsAuXYkCw_nY5jnsx_GWnTTDitEsGDvvWPbmQXftZ1MvH7lS3mHaR_z7DMwjltXfQCuaQMWIJT6Sz0E0YA
https://lh3.googleusercontent.com/0fQEstwagC-PABXvrGd5iWZsYwn8HQD4uqiS1YW3GrStq2FHUz98Uq0Tucw8rfKrhsAuXYkCw_nY5jnsx_GWnTTDitEsGDvvWPbmQXftZ1MvH7lS3mHaR_z7DMwjltXfQCuaQMWIJT6Sz0E0YA=s72-c
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/01/wizara-ya-mambo-ya-nje-yafafanua-kuhusu.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/01/wizara-ya-mambo-ya-nje-yafafanua-kuhusu.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy