Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye akizungumza na uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Mli...
 |
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Moses
Nnauye akizungumza na uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Mlimani Media wakati
alipofanya ziara kujionea utendaji kazi wake na changamoto wanazozipata katika
kutekeleza majukumu yao. Wapili kushoto, ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abass
NA BEATRICE LYIMO-MAELEZO
SERIKALI imevitaka vyombo vya habari nchini kuwa chachu ya mabadiliko katika
kipindi hiki ambacho nchi inaelekea katika uchumi wa kati.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye
katika ziara yake kwa vyombo vya habari vya Clouds, Mlimani na Azam, ziara
inayolenga kuimarisha mahusiano yaliyopo baina ya Serikali na vyombo vya habari
nchini.
“Serikali
ya Awamu ya Tano imejikita katika ajenda mbalimbali ikiwemo kutoka katika hali
ya uchumi tuliona nao sasa kuelekea uchumi wa kati hivyo vyombo vya habari
vinatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha suala hili linawafikia na
kuleta uelewa kwa wananchi”alisema Mhe. Nnauye.
Waziri
Nape alisisitiza kuwa, kumekuwa na mitazamo tofauti katika vichwa vya wananchi
au jamii kwa ujumla kuhusu suala zima la kuelekea uchumi wa kati, hivyo ni
jukumu la vyombo vya habari nchini kuweza kuwaelewesha nini maana halisi ya
uchumi unaolengwa kuufikiwa.
“tumesikia
ya kwamba uchumi wa nchi umekuwa kwa asilimia saba, mwananchi wa kawaida hawezi
kuwa na uelewa wa kujua ni vipi uchumi wa nchi unakuwa, hivyo vyombo vya
habari vina mchngo mkubwa katika kuifanya jamii kuwa uelewa juu ya ukuaji wa
uchumi” alisisitiza waziri Nape.
Mbali
na hayo Waziri Nape amesema kuwa vyombo vya habari ni chanzo cha wananchi kuwa
kitu kimoja katika kulinda amani ya nchi na utamaduni uliopo, hivyo vina budi
kuzidi kutunza utamaduni uliopo pamoja na kuwafanya wananchi kupenda utamaduni
wao.
Waziri
Nape alisisitiza kuwa vyombo vya habari viifanye jamii kwa ujumla kuwa na
utamadumi hasa wa utamaduni wa ulipaji wa kodi katika nyanja tofauti na kuwa
wazalendo kwa maendeleo ya nchi.
“sisi
kama wanahabari na vyombo vya habari kwa ujumla tunatakiwa kutengeneza vijana
ambao kwao kulipa kodi ni fahari, vijana ambao kazi kwao ni heshima pamoja na
kutengeneza vijana ambao hujivunia uzalendo wa nchi yao"Alisema Waziri
Nape.
Hata
hivyo Waziri Nape ameahidi kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya Serikali na
vyombo vya habari nchini katika nyanja tofauti ikiwemo utoaji wa habari muhimu
za utekelezaji wa Serikali katika kuleta maendeleo nchini.
|

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape
Moses Nnauye akizungumza na uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Clouds Media
group wakati alipofanya ziara kujionea utendaji kazi wake na changamoto
wanazozipata katika kutekeleza majukumu yao. Kulia kwake, ni Mkurugenzi
wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiangalia
jinsi habari zinavyoandaliwa wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo
vya habari kwenye studio za Azm TV
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses
Nnauye akiangalia sehemu mbalimbali za studio za Mlimani Tv na Redio iliyo
chini ya Mlimani Media wakati alipofanya ziara kujionea utendaji kazi wake na
changamoto wanazozipata katika kutekeleza majukumu yao.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses
Nnauye akiangalia sehemu mbalimbali za studio za Mlimani Tv na Redio iliyo
chini ya Mlimani Media wakati alipofanya ziara kujionea utendaji kazi wake na
changamoto wanazozipata katika kutekeleza majukumu yao.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape
Moses Nnauye akiangalia sehemu mbalimbali za studio za Azam Tv na Redio iliyo
chini ya Uhuru Production wakati alipofanya ziara kujionea utendaji kazi wake
na changamoto wanazozipata katika kutekeleza majukumu yao.

COMMENTS