Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali ( PAC) wakikagua utekelezaji wa Mradi wa Umeme katika kijiji cha Nyi...
Wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali ( PAC) wakikagua
utekelezaji wa Mradi wa Umeme katika kijiji cha Nyigo, Wilaya ya Mufindi mkoani
Iringa, Kamati hiyo inaongozwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini,
Dkt. Medard Kalemani pamoja na Watendaji kutoka Wakala ya Nishati
Vijijini (REA) na Shirika la Umeme nchini ( Tanesco).
Wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali,( PAC) wakimsikiliza
Meneja wa Tanesco Mufindi, wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa
Mradi wa Umeme Vijijini. Kamati PAC imeambatana na Naibu Waziri wa
Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani pamoja na watendaji kutoka
Wakala ya Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme nchini (Tanesco)
Jengo lenye moja
ya mashine za kusaga na kukoboa nafaka katika kijiji cha Nyigo, Mufindi
mkoani Iringa inayotumia umeme baada ya kuunganishwa na Mradi wa Umeme
Vijijini.
Mwenyekiti
wa Shirika lisilo la kiserikali linalohusika na utunzaji wa mazingira,
Mufindi Environmental Trust ( MUET), Godfrey Mosha akiwaonyesha Transfoma (haipo pichani) Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na Naibu Waziri wa Nishati na Madini
Dkt. Medard Kalemani. MUET imeunganishwa na huduma ya umeme, kupitia
mradi wa umeme vijijini ili kuendesha kituo cha kupumzikia wasafiri.


COMMENTS