Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Chiku Galawa akizungumza mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ...
Mkuu
wa Mkoa wa Songwe Mhe. Chiku Galawa akizungumza mbele ya
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) pale
kamati hiyo ilipofanya ziara ya kukagua miradi ya Umeme Songwe Vijijini,
katika Kikao kilichofanyika jana katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini
Songwe.
Kaimu
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC)
Mhe. Livingstone Lusinde akifafanua jambo mbele ya Wajumbe wa Kamati
hiyo, pale walipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya wa Ileje tayari ya
kwenda kukagua Mradi wa Umeme uliopo kijijini hapo, Kushoto wake ni
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Dkt. Medard Kalemani na Kulia
kwake ni Katibu Kamati wa Bunge anaehusika na Hesabu za Serikali (PAC)
Ndg. Asmin Kihemba na anaefuata ni Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mhe. Joseph Mkude. katika kikao kilichofanyika jana katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya
wa Ileje Mkoani Songwe.
Mkuu
wa Wilaya ya Ileje Mhe. Joseph M. Mkude akizungumza na
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) pale
kamati hiyo ilipomtembelea Ofisi kwake tayari kwa Ukaguzi wa mradi wa
umeme katika moja ya kijiji kilichopo Wilaya ya Ileje, Katika kikao
kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) walipotembelea
na Kukagua Mradi wa Umeme uliopo moja ya kijiji kilichopo Wilaya ya
Ileje Mkoani Songwe. (PICHA NA OFISI YA BUNGE).
COMMENTS