Meneja Mifumo ya Kielektroniki ya Forodha kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Tinkasimile Felix akipokea tuzo ya ubuni...
Meneja
Mifumo ya Kielektroniki ya Forodha kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) Tinkasimile Felix akipokea tuzo ya ubunifu wa mfumo
wa TANCIS kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kutoka Wizara ya
Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mindi
Kasiga. Mfumo huu wa TANCIA umeundwa kwa kuzingatia kanuni za hali ya
juu za kiteknolojia kwa lengo la kuongeza ufanisi, uharaka, uwazi na
uhakika katika usimamizi wa masuala ya forodha.
…………
Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) imepata tuzo kutoka Umoja wa Afrika (AU)
kutokana na mfumo wa Uondoaji Mizigo Bandarini (TANCIS) ambao unafanya
kazi kwa ufanisi na uharaka zaidi pamoja na kudhibiti mia nyaya rushwa.
Tuzo
hiyo imetolewa na Umoja wa Nchi za Afrika jijini Addis Ababa Ethiopia,
baada ya kufanyika shindano la Taasisi za Serikali za Umoja wa Nchi
hizo kutokana na kuboresha mifumo ya utendaji kazi katika taasisi zao.
Akizungumza
kwa niaba ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mindi Kasiga amesema kuwa TRA na Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya
Hifadhi ya Jamii(SSRA) ndiyo taasisi pekee za Serikali zilizoweza
kufanya vizuri katika ubunifu katika utendaji wa taasisi hizo.
“Tuzo
hizi zinatolewa na nchi za Umoja wa Afrika kwa taasisi za Serikali
ambapo hushindanishwa katika masuala ya ubunifu katika utendaji kazi wa
taasisi husika,” alisema Bi. Mindi.
Akizungumza
kwa niaba ya Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Alphayo Kidata, Mkurugenzi wa
Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi toka Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw.
Richard Kayombo alisema TRA imeshinda tuzo hiyo kutokana na ubunifu wa
mfumo wa TANCIS ambao umeundwa kwa kuzingatia kanuni za hali ya juu za
kiteknolojia kwa lengo la kuongeza ufanisi, uharaka, uwazi na uhakika
katika usimamizi wa masuala ya forodha.
Alisema
mfumo huu umeunganishwa na mifumo mingine ya TRA ni ya wadau muhimu
ambao wanahusika katika uondoshaji wa bidhaa katika udhibiti wa forodha.
“Mfumowa
TANCIS humwezesha mwagizaji wa bidhaa kufuatilia hatua iliyofikiwa
katika kuondosha bidhaa zake kwa kutumia simu ya kiganjani au kifaa
kingine chochote cha kielektroniki hivyo mfumo huu unarahisisha utoaji
huduma na kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato,” alisema Bw.
Kayombo.
Kwa
upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano toka Mamlaka ya Udhibiti wa
Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Bi. Sarah Kibonde alisema kuwa
taasisi yake imepokea tuzo hiyo ya ubunifu kwa kupitia mfumo wa kanzi
data yaTaifa ya Sekta ya Hifadhi ya Jamii.
Alisema
TRA iliwawezesha kupata taarifa zilizohusu walipaji kodi wa (PAYE)
ambazo zilifanikisha uchambuzi wa waajiri wasiochangia Mifuko ya Jamii.
TRA
na SSRA wameahidi kuendelea na ubunifu zaidi ili kuhakikisha
wanaendelea kubaki katika nafasi ya ushindi na kufanya vizuri zaidi
katika mashindano yajayo.
COMMENTS