WATANZANIA WASHAURIWA KUTUMIA NISHATI MBADALA KUNUSURU MAZINGIRA
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe akiongea wakati wa ufunguzi wa warsha ya kujadili mikakati ya kupunguza matumizi ya mkaa nchini katika kituo cha utalii Dar es Salaam leo.
HomeJamii

WATANZANIA WASHAURIWA KUTUMIA NISHATI MBADALA KUNUSURU MAZINGIRA

  Watanzania Washauriwa Kutumia Nishati Mbadala. Na Lilian Lundo Serikali itaendelea kuzuia matumizi ya mkaa na kuni ili kuendel...

TMA YAWAJENGEA UWEZO WANAHABARI UANDISHHI WA HABARI ZA HALI YA HEW
MAGAZETI YA MWANANCHI NA NIPASHE YAPEWA ONYO KALI
JKT MGULANI YACHANGIA DAMU HOSPITALI YA RUFAA YA TEMEKE NA KUFANYA USAFI

Watanzania Washauriwa Kutumia Nishati Mbadala.

WATANZANIA WASHAURIWA KUTUMIA NISHATI MBADALA KUNUSURU MAZINGIRA
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe akiongea wakati wa ufunguzi wa warsha ya kujadili mikakati ya kupunguza matumizi ya mkaa nchini katika kituo cha utalii Dar es Salaam leo.
Na Lilian Lundo

Serikali itaendelea kuzuia matumizi ya mkaa na kuni ili kuendelea kutunza mazingira na kuhifadhi uoto wa asili wa nchi yetu. 

Hayo yamesemwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe alipokuwa akisoma hotuba kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa leo Jijini Dar es Salaam katika warsha ya wadau kujadili namna na njia bora ya kupunguza matumizi ya mkaa kwa usimamizi endelevu wa mazingira nchini. 

Prof. Maghembe amesema kuwa Serikali itaendelea kurekebisha sheria ya gharama ya uzalishaji wa mkaa, ili nishati hiyo iwe na gharama ya juu na kuwafanya watanzania wahamie kwenye nishati nyingine kama vile gesi ambayo gharama yake ni rahisi. 

“Uchomaji wa mkaa unaharibu mazingira kwa kiwango kikubwa, ambapo miti inapokatwa joto huongezeka, kipindi hiki mvua za vuli zilitakiwa kuwa zinanyesha lakini mvua hizo hazinyeshi kutokana na ukataji miti uliokithili,” alifafanua Prof. Maghembe. 

Aliendelea kwa kusema kuwa ukataji wa miti umesababisha wanyamapori kuhama maeneo yao ya asili kwa ajili ya kutafuta maji na chakula.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba amesema kuwa nishati ya mkaa inaonekana kama nishati ambayo gharama yakeiko chini ukilinganisha na nishaati nyingine. Lakini mtu wa kipato ch chini anaweza kutumia mpaka shilingi 4,000 kwa siku kwa kununua mkaa gharama ambayo ni kubwa ukilinganisha na gharama za gesi. 

Nae Mkurugenzi wa kampuni ya ORXY -Tanzania Nick McAleer amesema kwamba watumiaji wa gesi wanaongezeka kila siku na mpaka sasa kampuni hiyo ina mawakala wapatao 1,000 wanaouza nishati hiyo. 

Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa nishati ya gesi gharama yake ni nafuu ukilinganisha na mkaa, vilevile utumiaji wa gesi unahifadhi mazingira na kuwaepushia watanzania magonjwa ya mapafu na kansa ambayo yanasababishwa na moshi wa mkaa na kuni. 

Aidha ameiomba Serikali kuondoa baadhi ya kodi hasa kwa mawakala ambao wanataka kuuza gesi kwani kwa kufanya hivyo kutaongeza idadi ya wauzaji na upatikanaji wa gesi kuwa ni wa rahisi nchi nzima.
 
Baadhi ya washiriki wakifuatilia hotuba ya mgeni Rasmi Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe Kassim Majaliwa katika warsha hiyo.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (katikati) Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, (Muungnao na Mazingira) January Makamba (kushoto) na Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Luhaga Mpina (kulia) pamoja na washiriki wengine wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa kwenye warsha hiyo jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Robert Okanda Blogspot)
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WATANZANIA WASHAURIWA KUTUMIA NISHATI MBADALA KUNUSURU MAZINGIRA
WATANZANIA WASHAURIWA KUTUMIA NISHATI MBADALA KUNUSURU MAZINGIRA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj7yuwzJs60BB3VSHHj29gjNi9KiJUqxkhCaAQb1wAD6zcEhPPTKHD-vhR0hy22-A1Jap34COBIFsqc6SGZZcDW169PhRzdVpgDIe07xvnw-MhX617yx4iCww0vlBwd8EFDdbLKQJbNbI4/s640/MAGEMBE.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj7yuwzJs60BB3VSHHj29gjNi9KiJUqxkhCaAQb1wAD6zcEhPPTKHD-vhR0hy22-A1Jap34COBIFsqc6SGZZcDW169PhRzdVpgDIe07xvnw-MhX617yx4iCww0vlBwd8EFDdbLKQJbNbI4/s72-c/MAGEMBE.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/11/watanzania-washauriwa-kutumia-nishati.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/11/watanzania-washauriwa-kutumia-nishati.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy