JKT MGULANI YACHANGIA DAMU HOSPITALI YA RUFAA YA TEMEKE NA KUFANYA USAFI
HomeJamii

JKT MGULANI YACHANGIA DAMU HOSPITALI YA RUFAA YA TEMEKE NA KUFANYA USAFI

  Mkuu wa    Kikosi  cha  Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)  namba 831 KJ Mgulani, Luteni Kanali, Zacharia Godfrey Kitani, akizungumza na wa...

TAARIFA KUHUSU UINGIZWAJI WA MIFUGO NCHINI TANZANIA
RAIS MSTAAFU MHE. DKT. JAKAYA KIKWETE AONGOZA MAHAFALI YA 47 YA CHUO KIKUU DAR ES SALAAM
SIKU YA TAKWIMU AFRIKA KUADHIMISHWA LEO


 Mkuu wa   Kikosi  cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) namba 831 KJ Mgulani, Luteni Kanali, Zacharia Godfrey Kitani, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu askari wa kikosi hicho kujitolea damu na kufanya usafi  katika maeneo mbalimbali ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 53 tangu lianzishwe Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),ambayo yatafikia kilele chake kesho kutwa nchini kote. 


 Jengo la Utawala la Hospitali hiyo.
 Mtaalamu wa Sayansi ya Maabara wa Hospitali hiyo, Bilal Babu akimtoa damu, Kijana  wa JKT,  Damiani Ambross wakati akichangia damu.
 Vijana wa JKT, wakisubiri kuchangia damu.
 Vijana wa JKT wakisukuma mkokoteni wenye matofari wakati wakifanya usafi katika hospitali hiyo.
 Vijana wa JKT wakiweka matofari katika eneo maalumu
 Usafi ukiendelea kufanywa.
 Mti ukikatwa.
 Matawi ya mti yakikatwa tayari kwa kuondolewa
 Usafi ukiendelea.
 Hapa ni kazi tu ya usafi.
 Mti uliokatwa ukisukumwa tayari kwa kuondolewa katika 
eneo hilo.
 Mti uliokatwa ukiondolewa eneo la tukio.
 Askari hao wa JKT wakiondoa matawi ya mti yaliyokatwa.
 Takataka zikiondolewa hospitali hapo kwa kutumia mifuko maalumu.
 Mtaalamu wa Sayansi ya Maabara wa Hospitali hiyo, Hassan Mwage akimtoa damu, Kijana  wa JKT,  Kafumu Godfrey Ambross wakati akichangia damu.
 Mtaalamu wa Sayansi ya Maabara wa Hospitali hiyo, Heri Shekighenda akimtoa damu, Kijana  wa JKT,  Kafumu Godfrey Ambross wakati akichangia damu.
 Vijana wa JKT wakijisajili majina yao kabla ya kutoa damu kwaajili ya kuchangia.
Takataka zikiondolewa.

Na Dotto Mwaibale

ASKARI wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kikosi namba 831 KJ Mgulani, wamejitolea kuchangia damu pamoja na kufanya usafi  katika maeneo mbalimbali ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 53 tangu lianzishwe Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),ambayo yatafikia kilele chake kesho kutwa nchini kote. 

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Mkuu wa Kikosi hicho Luteni Kanali Zacharia Godfrey Kitani alisema kila maadhimisho hayo yanapofanyika wamekuwa wakifanya shughuli za kijamii kama kufanya usafi na mwaka huu wameona wafanye usafi na kuchangia damu katika hospitali hiyo ili kusaidia  wananchi.

"Ni kawaida yetu katika kuadhimisha siku ya kuanzishwa jeshi letu sisi kama askari kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii katika maerneo tofauti tofauti kwa siku kadhaa leo hii tunafanya usafi katika Hospitali ya Temeke na kutoa damu na tutaendelea katika maeneo mengine hadi siku ya kilele cha maadhimisho haya hapo kesho kutwa" alisema Kitani.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Husna Msangi alisema msaada huo wa damu waliochangia askari hao utasaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na changamoto ya damu hospitalini hapo kutokana kuwa na mahitahi makubwa ya damu kwa wagonjwa.

Alisema mahitaji ya damu katika hospitali hiyo ni makubwa hivyo amewaomba wadau wengine wajitokeze kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watu ambao wataweza kupoteza maisha kwa kukosa damu.

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712727062)


Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: JKT MGULANI YACHANGIA DAMU HOSPITALI YA RUFAA YA TEMEKE NA KUFANYA USAFI
JKT MGULANI YACHANGIA DAMU HOSPITALI YA RUFAA YA TEMEKE NA KUFANYA USAFI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhYvmFyow_3QcWTB1aI2dP936MSvjHJQae0EHj5HHEDgl5hrqy0-RPqOru7PLDN4Lt1_yrsrsaAtM37T5h1CbeeSbY0OCw6PT088R_NbKBpc6Sb5le6A7-V4Yve-_rsEsCJkMXTahTmDXkM/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhYvmFyow_3QcWTB1aI2dP936MSvjHJQae0EHj5HHEDgl5hrqy0-RPqOru7PLDN4Lt1_yrsrsaAtM37T5h1CbeeSbY0OCw6PT088R_NbKBpc6Sb5le6A7-V4Yve-_rsEsCJkMXTahTmDXkM/s72-c/1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/08/jkt-mgulani-yachangia-damu-hospitali-ya.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/jkt-mgulani-yachangia-damu-hospitali-ya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy