Na Zuena Msuya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeridhishwa na utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini, unao...
Na Zuena Msuya
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za
Serikali (PAC) imeridhishwa na utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini, unaotekelezwa
na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika Awamu ya kwanza na ya Pili ili kuona
thamani halisi ya matumizi ya fedha za Serikali katika mradi huo.
Mwenyekiti wa PAC, Livingstone Lusinde
alisema hayo mkoani Iringa wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa
REA, katika vijiji na Taasisi mbalimbali zilizopitiwa na Mradi huo.
Lusinde alifafanua kuwa wameridhishwa na
utekelezaji wa miradi hiyo baada ya kuona miundombinu iliyotumika na maendeleo
ya wananchi katika maeneo ambayo
yamepitiwa na miradi hiyo.
" Tumepita katika vijiji mbalimbali hapa
Iringa ambayo nimepitiwa na REA, tumeona namna ambavyo mradi huo umetekelezwa
na tumeona miundombinu iliyotumika na maendeleo yake hivyo hatuna budi kusema
wazi kuwa tumeridhishwa na utekelezaji wa mradi huu", Alisema Lusinde.
Lusinde aliwasisitiza wakandarasi wanaotekeleza
Mradi wa Umeme vijijini, kutumia miundombinu imara inayokwenda sambamba na
thamani halisi ya matumizi ya fedha za Serikali katika kutekeleza wa miradi
hiyo ili kutimiza malengo yaliokusudiwa na kuondoa hasara za makusudi
zinazoweza kujitokeza.
Vilevile aliwataka wakandarasi hao kukamilisha
zoezi za kuwaunganisha na huduma ya umeme wananchi na Taasisi zilizoomba huduma
hiyo katika maeneo machache yaliyosalia ili kila mwananchi aliyeomba huduma hiyo
aweze kuipata kwa wakati na kuitumia.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nishati na
Madini DKt. Medard Kalemani alisema kuwa Awamu ya Tatu ya utekelezaji wa Mradi
wa Umeme wa Vijijini utashirikisha Viongozi Serikali za mitaa, Madiwani, Wabunge,
Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa.
Alifafanua kuwa lengo la kufanya hivyo ni
kutoa fursa kwa wananchi kutoa vipaumbele vya maeneo wanayotaka kufikiwa kwa
huduma ya umeme kwa wakati na kuvifikia vijiji vyote nchini.
" Mradi wa REA Awamu ya Tatu utakuwa
shirikishi, kwakuwa kabla ya mkandarasi kuanza kazi yake, atatakiwa kuwasiliana
na Viongozi wa Serikali ya mitaa, Madiwani, Wabunge, Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa
Mikoa ili wao watoe vipaumbe cha maeneo wanayotaka kufikiwa na mradi huo",
alifafanua Dkt. Kalema.
Dkt. Kalemani alibainisha kuwa utaratibu huo utawezesha
kuviunganisha vijiji vyote nchini na huduma ya umeme ili kutimiza azma ya
Serikali ya kufikia ya uchumi wa Kati ifikapo mwaka 2025.
Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC)
inafanya ziara ya kukagua Miradi ya Umeme Vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati
Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) kwa lengo
la kuona thamani hali matumizi ya fedha ya Serikali katika mradi huo.
![]() |
Wajumbe wa Kamati ya PAC, wakisikiliza taarifa ya Mkoa wa Iringa, kabla ya kuanza ziara ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme vijijini mkoani Iringa. |
![]() |
Wajumbe wa Kamati ya PAC, wakikagua Miradi ya Umeme Vijijini katika kijiji cha Nyamahana mkoani Iringa. |
![]() |
Add caption |
![]() |
Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, Livingstone Lusinde akiruka pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari Idodi, wakati wa ziara ya kukagua Miradi ya Umeme Vijijini. |
![]() |
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani akisalimiana na wanafunzi wa shule ya Sekondari Idodi, wakati wa ziara ya kukagua Miradi ya Umeme Vijijini. |
![]() |
Mjumbe wa Kamati ya PAC, Shally Raymond akisisitiza jambo kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Idodi, wakati wa ziara ya kukagua utelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini. |
COMMENTS