TPSC KUENDELEA KUWAJENGEA UWEZO WATUMISHI WA UMMA-WAZIRI KAIRUKI
HomeJamii

TPSC KUENDELEA KUWAJENGEA UWEZO WATUMISHI WA UMMA-WAZIRI KAIRUKI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Angellah Kairuki amesema kwamba serikali kupiti...

NAIBU WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU KAZI VIJANA NA AJIRA ATHONY MAVUNDE ATEMBELEA MIRADI YA VIJANA WAJASIRIAMALI MKOANI SONGWE
SERIKALI YAUNDA TUME KUBAINI CHANZO CHA MOTO JNIA
SERIKALI YAUNDA TUME KUCHUNGUZA KUUNGUA KWA CHUMBA CHA MIZIGO UWANJA WA NDEGE JIJINI DAR ES SALAAM


 TPSC KUENDELEA KUWAJENGEA UWEZO WATUMISHI WA UMMA-WAZIRI KAIRUKI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Angellah Kairuki amesema kwamba serikali kupitia Chuo Cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) itaendelea kuwajengea uwezo watumishi wa Umma ili waendane na kasi ya mabadiliko, changamoto na mahitaji ya sasa katika utumishi wa Umma.

Akiwasilisha taarifa ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala na Serikali za Mitaa Makao Makuu ya TPSC Mtaa wa Bibi Titi Jijini Dar es Salaam , Waziri Kairuki alisema kuwa mafunzo hayo ni muhimu sana kwa watumishi hao.
Aliongeza kuwa pia serikali inakamilisha mchakato wa mandalizi ya mafunzo ya lazima kwa watumishi wa umma nchini.Katika kuongeza ufanisi na tija wa chuo hicho, chuo kimejenga, kuhuisha na kusimika mifumo mbalimbali ya kusimamia utekelezaji wa majukumu.
“Baadhi ya mifumo hiyo ni mpango mkakati mwa mwaka 2016-2021,utekelezaji kikamilifu kwa mkataba wa huduma kwa mteja na kuanzishwa kwa dawati la malalamiko na kamati za uadilifu.Waziri alisema majukumu mengine ni kuendelea kusimika mifumo ya Tehema, miundombinu ya mtandao (LASN) , Mtandao wa serikali (Govnet) , mfumo wa simu za serikali (Voip) na mfumo wa barua pepe za Serikali (GSM).

Waziri Kairuki aliiambia kamati hiyo kuwa katika kuendeleza weledi wa watumishi wa Umma katika utunzaji wa kumbukumbu na Uhazili, Chuo kinatarajia kuanzisha shahada ya kwanza katika maeneo hayo mawili.“Rasimu ya Mitaala hiyo, imeshaandaliwa na kuwasilishwa baraza la Ithibati na Elimu ya Ufundi (NACTE) kwa ajili ya uhakiki na kuidhinishwa.” 
Alisema pia kuwa TPSC hutoa ushauri wa kitaalam kwa Wizara, Idara, Wakala za Serikali , Mamlaka za Serikali za Mitaa na sekta binafsi.Baadhi ya shauri hizo za kitaalam ni katika maeneo ya miundo na mifumo ya utumishi , mpango mkakati ,Mkataba wa huduma kwa mteja , tathmini na uchambuzi kazi , tathmini ya utoaji huduma katika utumishi wa umma na usimamizi wa mchakato wa ajira.
Waziri aliyataja baadhi ya majukumu ya Chuo kuwa ni kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa watumishi wa wa umma ili kuwajengea uwezo katika kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi. Mafunzo hayo ni katika Nyanja mbalimbali zikiwemo menejimenti ya usimamizi na rasilimali watu, menejimenti, uongozi na utawala, utunzaji wa kumbukumbu na usimamizi wa fedha .

Pia kinatoa mafunzo ya muda mrefu katika ngazi ya cheti na stashahada katika maeneo ya menejimenti na utawala, utunzaji wa kumbukumbu na uendeshaji wa ofisi, mafunzo ya uhazili,usimamizi wa fedha za umma , ununuzi na ugavi,huduma za maktaba utawala wa serikali za mitaa, sheria na teknolojia ya habari na mawasiliano. 
Chuo kina matawi sita mbayo ni Dar es Salaam, Mtwara, Tabora, Singida Tanga na Mbeya.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala na Serikali za Mitaa, Jasson Rweikiza (MB-Bukuba Vijijini) alikipongeza chuo hicho kwa jitihadaza zake za kuwaendeleza watumishi wa Umma na kutoa ushauri kwa Serikali ifungue tawi la chuo hicho Jijini Mwanza, ili kuwahudumia wakazi wa kanda ya Ziwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Angellah Kairuki(kushoto) akiwa na baadhi ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakimsikiliza kwa makini Kaimu Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Dkt.Henry Mambo wakati alipokuwa akiwaelezea maadeleo ya ukarabati wa majengo ya chuo hicho tawi la Magogonijijini Dar es Slaam, kamati ya bunge ilifanya ziara ya kikazi katika chuo hicho jana. 
Kaimu Mkuu wa Chuo Cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt.Henry Mambo, akisisitiza jambo mbelea ya wajumbe wa Kamati ya kudumu ya bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa kamati hiyo , Jasson Rweikiza,anayefuata ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Angellah Kairuki na kwa kwanza kulia ni Suzan Mlawi, Naibu Katimu Mkuu wa Wizara hiyo ya Ofisi ya Rais.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Angellah Kairuki (kulia) akifafanua jambo kwa wajumbe wakamati ya kudumu yabunge ya Utawala na Serikaliza Mitaa wakati walipofanya ziara ya kikazi katika makao makuu ya chuo hicho,Mtaa wa Bibi Titi, jijini Dar es Salaam, jana .Katikati ni Mwenyekiti wa kamati hiyo , Jasson Rweikiza na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Utumishiwa Umma Dkt.Henry Mambo.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Ino Communications Barnabas Lugwisha, akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Angellah Kairuki wakati wa ziara hiyo jana Chuo cha Utumishi wa Umma.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TPSC KUENDELEA KUWAJENGEA UWEZO WATUMISHI WA UMMA-WAZIRI KAIRUKI
TPSC KUENDELEA KUWAJENGEA UWEZO WATUMISHI WA UMMA-WAZIRI KAIRUKI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjCJBdPE3oYGjamzVTyK4aybs2v8Qn8Xy16YcpMe9zYmqK2_LJaakgTn_IRLu_hWXpX-QVTfzyryAqrbt5VEQAGezYBYoq6ZgwkFzeNV0YCgCGw6HRv9pTiT6zscDf7mgMx83haxOnZc7I/s640/DSC_0015.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjCJBdPE3oYGjamzVTyK4aybs2v8Qn8Xy16YcpMe9zYmqK2_LJaakgTn_IRLu_hWXpX-QVTfzyryAqrbt5VEQAGezYBYoq6ZgwkFzeNV0YCgCGw6HRv9pTiT6zscDf7mgMx83haxOnZc7I/s72-c/DSC_0015.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/01/tpsc-kuendelea-kuwajengea-uwezo.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/01/tpsc-kuendelea-kuwajengea-uwezo.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy