Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto), akiwa katika mazungumzo na mgeni wake ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa...
Waziri wa
Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto), akiwa katika
mazungumzo na mgeni wake ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, walipokutana
Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam.
Waziri wa
Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (katikati) pamoja na maafisa
waandamizi wa Wizara hiyo wakiwa katika mazungumzo na Mwakilishi Mkazi
wa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway,
Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw. Bhaswar
Mukhopadhway, (kulia) akisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa
yakitolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango
(hayupo pichani) wakati wa mazungumzo kati yao yaliyofanyika Makao Makuu
ya Wizara hiyo Jijini Dares salaam ambapo IMF imeipongeza Tanzania kwa
kusimamia vizuri ukuaji wake wa uchumi.
Ujumbe wa
Tanzania na Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF wakiwa katika
mazungumzo Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es
salaam, ambapo Shirika hilo limeahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania
ili kufikia maendeleo inayoyatarajia kwa manufaa ya Taifa na wananchi
wake kiuchumi na kijamii.
Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw. Bhaswar
Mukhopadhway, (kulia) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (hayupo pichani), Makao
Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dares salaam ambapo IMF imeipongeza Tanzania
kwa kusimamia kikamilifu ukuaji wake wa uchumi.
Mkurugenzi
wa Idara ya Sera wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Ollal, akisisitiza
jambo wakati wa mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.
Philip Mpango na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha
Duniani-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, walipokutana Makao Makuu ya
Wizara hiyo, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa
Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akizungumza jambo na mgeni
wake ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha
Duniani-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, (hayupo pichani), Makao Makuu ya
Wizara hiyo Jijini Dar es salaam.
Waziri wa
Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akizungumza jambo na mgeni
wake ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha
Duniani-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, (hayupo pichani), Makao Makuu ya
Wizara hiyo Jijini Dar es salaam.
Waziri wa
Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto), akiagana na mgeni
wake ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha
Duniani-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, baada ya kumalizika kwa
mazungumzo kati yao yaliyofanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar
es salaam, ambapo IMF, imesifu jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano,
katika kusimamia na kukuza uchumi wa Taifa.
……………..
Benny Mwaipaja,WFM-Dar es salaam
SERIKALI
imesema kuwa inatambua mchango mkubwa wa sekta binafsi katika kukuza
uchumi wa nchi na kuahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano na sekta hiyo
ili kuharakisha maendeleo ya wananchi kupitia sekta ya viwanda na
biashara.
Hayo
yamesema na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, alipokutana
na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la
Fedha Duniani-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, Makao Makuu ya Wizara hiyo
Jijini Dar es salaam.
Amesema
kuwa uchumi wa nchi unategemea sana sekta binafsi yenye nguvu na yenye
utulivu ambayo itachangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya nchi kwa njia
ya uwekezaji na ulipaji kodi.
Kwa
upande wake Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha
Duniani-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, amesema kuwa Shirika lake
limeridhika na kiwango kikubwa cha ukuaji wa uchumi wa Tanzania miongoni
mwa nchi za Afrika na kwamba wanatarajia kuona uchumi huo ukiendelea
kukua zaidi kwa ushirikiano na sekta binafsi.
Ametaja
sifa za ukuaji huo kuwa ni pamoja na kuimarishwa kwa ukusanyaji wa kodi,
udhibiti wa mfumuko wa bei na thamani ya shilingi, uwajibikaji na
pamambano dhidi ya rushwa, ufisadi, na utekelezaji mzuri wa Bajeti ya
serikali.
Hivi
karibuni Bodi ya Wakurugenzi ya IMF ilitoa taarifa yake ya mapitio ya
mwenendo wa uchumi wa Tanzania na kueleza kuridhika kwake na uimara wa
uchumi huo baada ya kutoyumba katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016 na
kueleza kuwa utaendelea kukua kwa wastani wa asilimia 7 kama
ilivyopangwa.
Shirika
la Kimataifa la Fedha Duniani ni chombo cha kimataifa kinachosaidia
ukuaji wa uchumi wa nchi wanachama wake kwa kuweka mikakati na
kuzikopesha fedha kwaajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo ya
kiuchmi na kijamii ikiwemo, elimu, afya, miundombinu, nishati na miradi
mingine kadha wa kadha.

COMMENTS