Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akielezea jinsi upasuaji wa Magonjwa ya Moyo unavyofany...

Mkurugenzi
wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akielezea
jinsi upasuaji wa Magonjwa ya Moyo unavyofanyika katika taasisi hiyo
wakati wageni kutoka Chuo kikuu cha Witwatersrand cha Nchini Afrika ya
Kusini walipotembelea wodi aliyokuwa amelazwa mmoja wa wagonjwa
aliyefanyiwa upasuaji. Kutoka kulia ni Prof. Martin Valler, akifuatiwa
na Afisa Muuguzi Roger Kibula, watatu kulia ni Prof. Simon Nemutandani
na wa pili kushoto ni Dkt. Marion Bergman.

Daktari
bingwa wa Magonjwa ya Moyo na Mhadhili kutoka chuo Kikuu kishiriki cha
Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) Prof. Johnson Rwakatare akimuonyesha
vipimo vya moyo (ECHO) Prof. Martin Valler Mkuu wa Kitivo cha Sayansi ya
Afya wa Chuo kikuu cha Witwatersrand cha Nchini Afrika ya Kusini
alipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete hivi karibuni.

Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi
akiwaeleza wataalamu wa afya kutoka Chuo Kikuu cha Minnesota cha nchini
Marekani huduma za matibabu ya moyo wanazozitoa wakati walipoitembelea
Taasisi hiyo hivi karibuni. Picha na Anna Nkinda - JKCI.

Mkurugenzi
wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi
akiwaonyesha wageni kutoka Chuo kikuu cha Witwatersrand cha Nchini
Afrika ya Kusini sehemu ya malipo ambapo wagonjwa wanalipia huduma.
Wageni hao walitembelea Taasisi hiyo hivi karibuni ili kuona huduma za
matibabu ya moyo wanazozifanya pia waliahidi kuimarisha mahusiano kati
yao hii ikiwa ni pamoja na kutoa ufadhili wa masomo kwa madaktari
wataokwenda kusoma katika chuo hicho.

Mkurugenzi
wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi na Prof.
Martin Valler Mkuu wa Kitivo cha Sayansi ya Afya wa Chuo kikuu cha
Witwatersrand cha Nchini Afrika ya Kusini wakiangalia jinsi upasuaji wa
bila kufungua kifua (Catheterization) unavyofanyika katika chumba Cath
Lab kilichopo katika Taasisi hiyo.

COMMENTS