Balozi Mbelwa Kairuki, China Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, Brazil Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe...
Balozi Mbelwa Kairuki, China
Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, Brazil
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 19 Januari, 2017
amewateua Mabalozi watano kuiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali.
Taarifa iliyotolewa na
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imewataja Mabalozi walioteuliwa na vituo
vyao vya kazi kama ifuatavyo;
1. Balozi Mbelwa Brighton Kairuki ameteuliwa
kuiwakilisha Tanzania Beijing – China.
2. Balozi George Kahema Madafa ameteuliwa
kuiwakilisha Tanzania Rome – Italy.
3. Balozi Emmanuel John Nchimbi ameteuliwa
kuiwakilisha Tanzania Brasilia – Brazil.
4. Balozi Fatma M. Rajab ameteuliwa kuiwakilisha
Tanzania Doha- Qatar.
5. Balozi Prof. Elizabeth Kiondo ameteuliwa
kuiwakilisha Tanzania Ankara – Uturuki.
6. Balozi Dkt. James Alex Msekela ameteuliwa
kuiwakilisha Tanzania Geneva – Umoja wa Mataifa.
Mabalozi hawa
wataapishwa kesho tarehe 20 Januari, 2017 saa 10:30 Jioni Ikulu Jijini Dar es
Salaam.
Wakati huo huo,
Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Muhidin Ally Mboweto kuwa Balozi.
Tarehe ya kuapishwa na
kituo cha kazi cha Bw. Muhidin Ally Mboweto kitatangazwa baadaye.
COMMENTS