MSD YASEMA UPATIKANAJI WA DAWA NCHINI UMEIMARIKA
Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa (MSD) Laurean Bwanakunu akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa ya kuimarika kwa upatikanaji wa dawa nchini. Kulia ni Ofisa Mwandamizi wa Idara Habari Maelezo, Zamaradi Kawawa.
HomeJamii

MSD YASEMA UPATIKANAJI WA DAWA NCHINI UMEIMARIKA

Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa (MSD) Laurean Bwanakunu akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa ya ...












Na Dotto Mwaibale

MKURUGENZI wa Bohari ya Dawa (MSD) Laurean Bwanakunu amesema hali ya upatikanaji wa dawa kwasasa imeboreshwa kutoka asilimia 54 iliyokuwepo mwaka jana, hadi kufikia asilimia 74 hivi sasa. 

Ameuhakikishia umma uwa upatikanaji wa dawa utaimarika mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu hadi kufikia asilimia 90.

Amesema kwa sasa kati ya aina za dawa muhimu 135 zinazohitajika kuwepo MSD dawa aina 100 zinapatika kwenye maghala ya MSD

Mkurugenzi wa MSD, Bwanakunu ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari, Dar es Salaam leo Ukumbi wa Idara ya habari Maelezo, alipokuwa kwenye mkutano ulioandaliwa na idara katika jukumu lake la kutoa nafasi kwa Idara na Taasisi za serikali kuelezea utekelezaji wa majukumu yao.

Katika hatua nyingine, Bwanakunu ameeleza kuwa, MSD imefanikiwa kurejesha Maghala iliyokuwa imekodi kwa ajili ya kuhifadhia vifaa tiba, hatua ambayo inaokoa sh.Bilioni 4 ambazo zilikuwa zikilipwa kama kodi kila mwaka. 

Ameongeza kuwa, tayari wamekabidhiwa kiwanja eneo la Luguruni, wilayani Ubungo walichopewa na Rais John Magufuli ambacho kitatumika kujenga ofisi za Kanda ya Dar es Salaam.

Kuhusu maduka, ameeleza kuwa wiki ijayo wanatarajia kuzindua  duka la dawa la MSD mkoani Katavi, ambalo litaifanya MSD kuwa na jumla ya maduka Saba, mengine yakiwa mkoani Arusha, Dar es Salaam, Mwanza, Lindi, Geita naMbeya. 

Akijibu swali juu ya ukosefu wa vifaa vyakujifungulia wajawazito Mkurugenzi Mkuu amesema vipo vyakutosha,na  zabuni ya manunuzi ya vifungashio kwa ajili ya vifaa hivyo vyakujifungulia iko katika mchakato wa kumpata mshitiri. 

Ameeleza kuwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu anaangalia namna ya kuwawezesha akina mama wasio kuwa na uwezo wakununua vifaa hivyo ambapo
utaratibu huo atautoa baadae.

Kwa sasa MSD inanunua dawa na vifaa tiba moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji, ilikuhakikisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba unakuwaendelevu na kupunguza gharama za ununuzi wa dawa hizo, ambazo asilimia 80 zinatoka nje ya nchi.


Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MSD YASEMA UPATIKANAJI WA DAWA NCHINI UMEIMARIKA
MSD YASEMA UPATIKANAJI WA DAWA NCHINI UMEIMARIKA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhW1JVl0S0leo4FzPVYG7JFvHTxlLbXmtT4s9W7l0uWmdYJ4keC-h60oHy6EAfIDkOL4K2ww44sS4BnsJ_wmnI-6TqZUpNpCWtWrapHtLSvHYdlgqp9ncf8KLBt2uuJZyyo9RtOOOXOG-lM/s640/zamaradi.PNG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhW1JVl0S0leo4FzPVYG7JFvHTxlLbXmtT4s9W7l0uWmdYJ4keC-h60oHy6EAfIDkOL4K2ww44sS4BnsJ_wmnI-6TqZUpNpCWtWrapHtLSvHYdlgqp9ncf8KLBt2uuJZyyo9RtOOOXOG-lM/s72-c/zamaradi.PNG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/01/msd-yasema-upatikanaji-wa-dawa-nchini.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/01/msd-yasema-upatikanaji-wa-dawa-nchini.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy