Katibu Mkuu wa Chama cha Tanzania-China Friendship Promotion Association Bw.Joseph kahama akiongea na waandishi wa habari (hawa...
Katibu
Mkuu wa Chama cha Tanzania-China Friendship Promotion Association
Bw.Joseph kahama akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya
matembezi ya kupinga ujangili wa Tembo (Walk for Elephant 2017)
yatakayofanyika kesho asubuhi kuanzia saa 12 asubuhi kuanzia Ubalozi wa
China mpaka Hoteli ya Sea Cliff.Kushoto kwake ni Hongxiang Huang kutoa
China House.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Tanzania-China Friendship Promotion Association
Bw.Joseph kahama akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya
matembezi ya kupinga ujangili wa Tembo (Walk for Elephant 2017)
yatakayofanyika kesho asubuhi kuanzia saa 12 asubuhi kuanzia Ubalozi wa
China mpaka Hoteli ya Sea Cliff.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Tanzania-China Friendship Promotion Association
Bw.Joseph kahama akionyesha tangazo lenye ujumbe wa kuhimiza matembezi
ya ku kupinga ujangili wa Tembo (Walk for Elephant 2017) yatakayofanyika
kesho asubuhi kuanzia saa 12 asubuhi kuanzia Ubalozi wa China mpaka
Hoteli ya Sea Cliff. Kushoto kwake ni Hongxiang Huang kutoa China House.Picha na Daudi Manongi-MAELEZO.
Na Frank Shija-MAELEZO.
MKAPA
kuongoza matembezi ya hiari ya kilomita tano yanayojulikana kama Walk
for Elephant Dar es Salaam 2017yatayofanyika kesho kuanzaia saa 12
asubuhi yaikianzia Ubalozi wa China hadi Sea Cliff Hotel.
Hayo
yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Urafiki baina ya Tanzania na
China (TCFPA) Joseph Kahama alipokuwa akiongea na waandishi wa habari
kuhusiana na matembezi hayo leo jijini Dar es Salaam.
Kahama amesema kuwa yana lengo la kuonyesha umoja katika kupinga ujangili unaofanywa dhidi ya Tembo.
“Tunatarajia
kuwa na matembezi ya kwa ajili ya kupinga ujangili dhidi ya Tembo
ambapo wageni wetu mashuhuri wanatarajiwa kuwa Marais wastaafu Mzee Ali
Hassan Mwinyi na Mzee Mkapa atakayepokea matembezi hayo katika Hotel ya
Sea Cliff,” alisema Kahama.
Aliongeza
kuwa zaidi ya watu 550 wamethibitisha kushiriki katika matembezi hayo
wakiwemo baadhi ya watu maarufu kama vile Jokate Mwigelo, Mrisho Mpoto
na wasanii wengine.
Aidha
Katibu Mkuu huyo alisema kuwa Chama cha Urafiki baina ya Tanzania na
China(TCFPA) imeanzishwa kwa nia ya kudumisha urafiki na uhusiano baina
ya raia wa nchini hizo mbili.
Akijibu
swali la mwandishi wa habari aliyetaka kujua ni kwanin china imeamua
kusaidia katika vita dhidi ya ujangili ili hali inatajwa kuwa miongoni
mwa soko kubwa la bidhaa za meno ya Tembo, Kahama alisema kuwa Serikali
ya China haiku tayari kuona nchi yake inatajwa kama soko la meno ya
Tembo ndiyo maana Rais Xi Jinping wa China na Barrack Obama wa Marekani
wamewahi kutoa tamko la pamoja la kupinga ujangili na ni kosa la jina
kwa rai wa China kukamatwa na nyara hizo.
Chama
hicho kimekusudia kuifanya tarehe 14 mwezi wa kwanza kila mwaka kuwa
siku ya matembezi ya Walk for Elphant Dar es Salaam 2017 ili kujenga
utamaduni endelevu wa kupinga ujangili.
COMMENTS