Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasikiliza Mawaziri wa Nishati kutoka Tanzania na Za...
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiwasikiliza Mawaziri wa Nishati kutoka Tanzania na Zambia
wakati wa kikao cha kupokea taarifa ya tathmini ya ujenzi wa bomba jipya
la mafuta safi kutoka Tanzania mpaka Zambia, Mawaziri hao ni Waziri wa
Nishati na Madini wa
Tanzania Mhe.Profesa Sospeter Muhongo (kulia) na Waziri wa Nishati wa
Zambia Bw. David Mabumba (kushoto), Ikulu jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Nishati wa Zambia Bw. David Mabumba (kushoto) mara baada ya kupokea taarifa ya tathmini ya ujenzi wa bomba jipya la mafuta safi litakalotoka Dar es Salaam, Tanzania mpaka Ndola, Zambia, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Ujumbe wa Tanzania na Zambia ambao ulifanya ziara ya kukagua pampu na bomba la mafuta la TAZAMA kutoka Ndola, Zambia mpaka Dar es Salaam Tanzania wakiongozwa na Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Sospeter Muhongo na Waziri wa Nishati wa Zambia Bw. David Mabumba ambapo walifanya tathmini ya ujenzi wa bomba jipya la mafuta safi litakalotoka Dar es Salaam, Tanzania mpaka Ndola, Zambia.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI




COMMENTS