Watumiaji wa simu za mkononi wameaswa kutokutoa namba za siri za simu zao wanapopigiwa simu au kutumiwa ujumbe mfupi yaani SMS. Ak...
Watumiaji wa simu za mkononi wameaswa kutokutoa namba za siri za simu zao wanapopigiwa simu au kutumiwa ujumbe mfupi yaani SMS. Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Bi. Jacquiline Materu, alisema“Natoa wito kwa wateja wetu kuwa makini na matapeli wanaowapigia simu na kuwafahamisha kuwa wameshinda fedha za Promosheni ya Nogesha Upendo au bonasi ya M-Pesa.
Vodacom Tanzania haina utaratibu wa kuwapigia simu wateja kuhusiana na mgao wa fedha za bonasi ya M-Pesa bali inatoa mgao huo kwa kadri ya mteja alivyotumia huduma hii na rekodi zote za matumizi kampuni inazo sambamba na utaratibu uliowekwa na Benki Kuu.
Materu alisema kampuni inawapigia simu wateja wa Promosheni ya Nogesha Upendo tu na kuwajulisha kuwa wameshinda na fedha zao hutumwa moja kwa moja kwa njia ya M-pesa ndani ya masaa 48 bila kuwataka wateja hao kutoa taarifa zozote za siri juu ya namba zao. Wengine wanaowapigia simu wateja kuhusiana na bonasi ni matapeli ambao wanataka kupata namba za siri na kuwatajia kiasi gani cha fedha mlizonazo ili wapate fursa ya kuwaibia fedha,” alisema Materu.
Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Bi. Jacquiline Materu
COMMENTS