Meneja wa shamba hilo, Bakar Mohamed akielezea kuhusu shamba hilo. Waandishi wa habari, Lucy Ngowi wa gazeti la Habari...
Meneja wa shamba hilo, Bakar Mohamed akielezea kuhusu
shamba hilo.
Waandishi
wa habari, Lucy Ngowi wa gazeti la Habari Leo (kushoto), Dotto Mwaibale
wa Jambo Leo (katikati) na Fatma Abdu wa Daily News wakijadiliana jambo
katika shamba hilo la majaribio.
Mwonekano wa shamba hilo.
Mjumbe wa Kamati hiyo, Mhandisi Kissina kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji, akiangalia hindi lililotokana na teknolojia hiyo.
Mshauri
wa mradi wa Wema, Dk. Alois Kullaya (kulia), akitoa maelezo kwa wajumbe
wa Kamati ya Taifa ya Matumizi Salama ya Bioteknolojia (NBC), kuhusu
matumizi ya Teknolojia ya Uhandisi Jeni (GMO) walipotembelea shamba la
majaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi
jeni (GMO) chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha
Makutupora mjini Dodoma leo.
Safari ya kuelekea kuangalia shimo la kuchomea uchafu mbalimbali baada ya kufanya utafiti ikiendelea. |
Wajumbe wa kamati hiyo na watafiti wa kilimo wakiangalia shimo la kuchomea uchafu mbalimbali baada ya kufanya utafiti huo.
Wajumbe wa kamati hiyo na watafiti wa kilimo wakiangalia shimo la kuchomea uchafu mbalimbali baada ya kufanya utafiti huo.
Mlinzi wa shamba hilo, Mbisi Masinga akiwa kazini. |
Watafiti wa Kilimo na Wajumbe wa Kamati ya NBC wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya shamba hilo.
Na Dotto Mwaibale, Dodoma
KAMATI
ya Taifa ya Matumizi Salama ya Bioteknolojia (NBC) imeridhishwa na
matumizi ya Teknolojia ya Uhandisi Jeni (GMO) yenye lengo la kuwakwamua
wakulima nchini.
Wajumbe
wa kamati hiyo wakizungumza kwa nyakati tofauti na waandishi wa habari
wakati walipotembelea shamba la majaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa
kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni (GMO) chini ya mradi wa Wema katika
Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma leo walisema
hatua iliyofikiwa na watafiti hao ni kubwa hivyo haipaswi kuachwa
ikapotea bure.
Elisa
Moses kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe ambaye ni mjumbe wa NBC
alisema teknolojia hii ya bioteknolojia ni nzuri na inaonesha uhalisia
halisi na inaweza kusaidia changamoto za ukosefu wa chakula iliyopo
nchi.
"Binafsi
nimefurahi kujionea hali halisi ya teknolojia hii hasa ninapoyaona
mahindi haya ya GMO yalivyomakubwa kwani ni muhimu sana katika
kukabiliana na ukame uliopo sehemu kubwa nchini" alisema Moses.
Mjumbe
mwingine wa kamati hiyo kutoka Chemba ya Wanyabiashara Wenye Viwanda na
Kilimo, Magdalene Mkocha alisema wamefurahi kuona jambo walilolipitisha
linafanyiwa kazi vizuri na linaleta matumaini makubwa kutokana na
matokeo ya jaribio hilo.
Alisema
wadau wa sekta binafsi wanasubiri kwa hamu kuhusu matokeo hayo baada ya
kuthibitishwa na takwimu za kisayansi kwani kwa kuangalia kwa macho
mahindi yanaonekana ni bora zaidi.
Ofisa
Habari na Mawasiliano wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Kanda ya Kati
Dodoma, Sebastian Kandira alisema hapo awali tafiti hizo zilikuwa
hazifikishwi kwa wakulima ndio maana zilikuwa hazieleweki vizuri lakini
hivi sasa wameanza kuzielewa kupitia vyombo mbalimbali vya habari.
Mkurugenzi
wa Utafiti na Maendeleo Kanda ya Kati, Leon Mroso alisema wakati
wanaanza majaribio hayo kulikuwa na changamoto nyingi kutokana na wadau
kutokuwa na uelewa hasa kwa mahindi yaliyobadilishwa vinasaba kikubwa ni
mshukuru Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Charles Tizeba kwa kufika
katika shamba hili la majaribio ambalo tulipanda mahindi Oktoba 5, mwaka
jana na kutupa faraja kuwa kuna kila sababu ya kuharakisha matumizi ya
teknolojia hiyo ili iweze kutumika kama zinazofanya nchi zingine
zinazofanya tafiti za namna hiyo.
Wajumbe
wa Kamati ya Taifa ya Matumizi Salama ya Bioteknolojia (NBC), waandishi
wa habari na watafiti wakielekea ukumbuni walipowasili Kituo cha
Utafiti wa Kilimo cha Kanda ya Kati Makutupora mkoani Dodoma leo asubuhi
kuangalia shamba la majaribio la mahindi yaliyotokana na teknolojia ya
uhandisi jeni (GMO)
Mkurugenzi
wa Utafiti na Maendeleo wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Hussein
Mansour akizungumza katika mkutano huo wakati akiwakaribisha wajumbe wa
NBC katika kituo hicho cha utafiti wa kilimo cha Makutupora cha mkoani
Dodoma.
Mshauri
wa mradi wa Wema, Dk. Alois Kullaya (kkushoto), akitoa maelezo mafupi
kwa wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Matumizi Salama ya Bioteknolojia
(NBC), kabla ya kuingia katika shamba la majaribio la mahindi
yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni (GMO) chini ya
mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini
Dodoma leo.
COMMENTS