Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (wa kwanza kulia), akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na ujumbe kuto...

Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (wa kwanza kulia),
akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na ujumbe kutoka nchini
Denmark, ukiongozwa na Waziri wa nchi anayeshughulikia Sera, Bw. Martin
Hermann, walipokutana Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango Jijini
Dar es salaam.
Ujumbe
wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip
Mpango na Ujumbe kutoka Serikali ya Denmark ukiongozwa na Waziri wa
Nchi-Sera, Bw. Martin Hermann, walipokutana kwa mazungumzo kuhusu
ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, Mkutano uliofanyika Makao Makuu ya
Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Nchi anayehusika na masuala ya Sera, Bw. Martin Hermann (kulia)
akiwa na ujumbe wake wakati wa mazungumzo kati yake na Waziri wa Fedha
na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (hayupo pichani), Makao Makuu ya
Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es salaam, ambapo nchi hizo
zimekubaliana kuendeleza ushirikiano utakaojikita katika masuala ya
uwekezaji na biashara kwa faida ya pande zote mbili. Kushoto ni Balozi
wa Denmark hapa nchini Bw. Einar Jansen.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto), akisisitiza
jambo wakati wa mkutano wake na ujumbe kutoka nchini Denmark, ukiongozwa
na Waziri wa nchi anayeshughulikia Sera, Bw. Martin Hermann, (hayupo
Pichani) walipokutana Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini
Dar es salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw.
Doto James.
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (kulia) na Katibu Mkuu
wa Wizara hiyo Bw. Doto James, wakifuatilia kwa umakini mazungumzo kati
ya Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango na Waziri wa Nchi
anayeshughulika na masuala ya Sera wa Denmark, Bw. Martin Hermann
(hawapo pichani), Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar
es salaam.
Waziri
wa Nchi anayehusika na masuala ya Sera kutoka Denmark, Bw. Martin
Hermann (kushoto) akimkabidhi Dkt. Mpango, nyaraka za kampuni
zinazoonesha nia ya kuwekeza Tanzania katika Sekta ya Gesi na Mafuta
wakati akiongoza ujumbe wa nchi hiyo katika mazungumzo kati yake na
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kulia), Makao Makuu
ya Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (katikati) akiangalia nyaraka
alizokabidhiwa na Waziri wa Nchi wa Serikali ya Denmark anayehusika na
Sera, Bw. Martin Hermann, wakati wa mazungumzo kati yao yaliyojikita
katika masuala ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya
nchi hizo mbili. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Doto James na
kulia kwa Waziri Dkt. Mpango, ni Naibu Katibu Mkuu Dkt. Khatib Kazungu.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (wa pili kushoto) akiwa na
wageni wake kutoka Serikali ya Denmark wakiongozwa na Waziri wa Nchi
anayehusika na Sera, Bw. Martin Hermann (kushoto), baada ya kumalizika
kwa mazungumzo kati yao ambapo masuala kadhaa yamejadiliwa ikiwemo
kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na kijamii hususan katika uwekezaji na
biashara, mazungungo yaliyofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na
Mipango, Jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto) akipeana mkono
wa shukurani na mgeni wake kutoka Serikali ya Denmark, Waziri wa Nchi
anayehusika na Sera, Bw. Martin Hermann (kushoto), baada ya kumalizika
kwa mazungumzo kati yao yaliyogusa Nyanja mbalimbali za kiuchumi na
kijamii hususan katika uwekezaji na biashara, mazungunzo yaliyofanyika
makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto) akiwasindikiza
wageni wake kutoka nje ya jengo la Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na
Mipango, Jijini Dar es salaam baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati ya
ujumbe wa Serikali ya Denmark na Tanzania uliolenga kuimarisha uhusiano
katika masuala ya uwekezaji na biashara.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WFM).
……………….
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es salaam
SERIKALI
ya Denmark imeahidi kuwashawishi wawekezaji wakubwa kutoka nchini humo
kuja kuwekeza hapa nchini katika sekta za Kilimo, Mifugo, Uvuvi,
Viwanda, Bandari, Gesi na Mafuta.
Ahadi
hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam na Waziri wa Nchi wa Serikali ya
Denmark anayeshughulikia Sera, Bw. Martin Hermann, alipokutana na
kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango,
Makao Makuu ya Wizara hiyo.
Bw.
Hermann alielezea kufurahishwa kwake na namna Serikali ya Awamu ya Tano
ilivyojipanga kuwatumikia wananchi wake kwa kuwaletea maendeleo ya
haraka ya kiuchumi pamoja na kuimarisha uwajibikaji, mapambano dhidi ya
rushwa na ufisadi, na kusema kuwa nchi yake inaunga mkono juhudi hizo.
Alisema
kuwa nchi yake itasaidia juhudi hizo kwa kuzishawishi kampuni kubwa
zenye mitaji na uwezo wa kiteknolojia kutoka sekta binafsi ili zije
ziwekeze hapa nchini na hivyo kushiriki katika kukuza uchumi wa nchi.
Amesisitiza
pia umuhimu wa serikali kuwekeza juhudi kubwa katika kuendeleza kilimo
kwa kuwa sekta hiyo inaweza kuchochea na kutoa mchango mkubwa na wa
haraka wa ustawi na maendeleo ya wananchi.
Aidha,
Bw. Hermann, ambaye aliambatana na Balozi wa Denmark hapa nchini, Bw.
Einar Jensen, amesifu utendaji mzuri wa Rais Mhe. Dkt. John Magufuli
katika mapambano dhidi ya vitendo vya ufisadi ikiwemo rushwa na
kuishauri Serikali kuweka mfumo wa vita hiyo utakaokuwa endelevu.
Kwa
upande wake Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, alisema
Serikali inathamini mchango mkubwa wa Denmark katika kukuza uchumi na
maendeleo ya Taifa kwa ujumla kwa kusaidia miradi ya maendeleo na
ushauri wa kisera.
“Katika
kipindi cha zaidi ya miaka 50 ya uhusiano kati ya nchi hizi mbili
tumeshuhudia Serikali ya Denmark ikichangia maendeleo yetu katika nyanja
zinazokwenda sambamba na vipaumbele vya maono ya mipango yetu ya
maendeleo katika sekta za fedha, miundombinu, kilimo, afya na
elimu”alisisitiza Dkt. Mpango.
Dkt.
Mpango aliishauri nchi hiyo kwamba mwelekeo wa uhusiano huo sasa uwe
katika kushirikiana kiuchumi kwa kuhamasisha uwekezaji na biashara kati
ya pande hizo mbili.
Alifafanua
kuwa amejaribu kutafuta takwimu za kiwango cha uagizaji na uingizaji wa
bidhaa kati ya Tanzania na Denmark lakini cha kusikitisha hakuna
biashara hiyo jambo ambalo amesema inabidi lilisisitizwe katika mfumo
mpya wa ushirikiano kwa kuwa kuna fursa nyingi zinazoweza kusaidia pande
zote mbili kiuchumi.
Alisisitiza
kuwa mwelekeo huo ni muhimu utiliwe mkazo sambamba na jitihada za
Serikali za kuboresha mazingira ya kufanya biashara na kuwekeza hapa
nchini huku akitoa wito kwa kampuni za Denmark zilizopo hapa nchini pia
kuvuta kampuni nyingine kutoka nchini mwao kuja kuwekeza Tanzania.
Dkt.
Mpango, amewakaribisha wawekezaji hao kuwekeza katika katika sekta za
ufugaji wa samaki, ujenzi wa viwanda vya kuchakata samaki, ufugaji wa
ng’ombe wa kisasa na viwanda vya kusindika nyama na maziwa, hatua
itakayo saidia kukuza mitaji, kuongeza tija katika sekta hizo na ajira
kwa kundi kubwa la vijana.
Kuhusu
ushauri uliotolewa na Waziri wa nchi wa Denmark anaye shughulikia Sera,
Bw. Martin Hermann wa kujenga mfumo endelevu wa kupambana na rushwa na
ufisadi, Dkt. Mpango amesema kuwa Serikali imeanzisha mahakama maalumu
ya mafisadi ambayo anaamini ni moja ya ujenzi wa mifumo hiyo endelevu ya
kupambana na vitendo hivyo.

COMMENTS