COSATO CHUMI ATATUA TATIZO LA MASHUKA KATIKA ZAHANATI, VITUO VYA AFYA NA HOSPITALI ZA JIMBO LA MAFINGA MJINI
HomeJamii

COSATO CHUMI ATATUA TATIZO LA MASHUKA KATIKA ZAHANATI, VITUO VYA AFYA NA HOSPITALI ZA JIMBO LA MAFINGA MJINI

Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akikabidhi mashuka kwenye moja ya Zahanati ilikuwa na upungufu wa mashuka...

MASHINDANO YA SCOUT KANDA YA AFRIKA MASHARIKI YAFANYIKA ARUSHA
UNICEF YAADHIMINISHA MIAKA 70 TANGU KUANZISHWA, SERIKALI YAIPONGEZA KWA KUSAIDIA WATOTO
IOP WAMEMA NDOA ZA UTOTONI ZINAZIDI KUONGEZEKA MKOANI IRINGA




Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akikabidhi mashuka kwenye moja ya Zahanati ilikuwa na upungufu wa mashuka katika kata ya Isalavanu wakati wa ziara yake ya kukagua na kugundua changamoto za zahanati za jimbo la mafinga mjini.

 Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi kushoto akiwa na katibu wake pamoja na mfanyakazi wa zahanati matanana wakati wa ziara yake.
 

 Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akiwasalimia wananchi wa kata ya Isalavanu wakati wa ziara yake.
 

Mbunge wa mafinga mjini akitandika moja ya shuka kati ya mashuka aliyoyagawa katika zahanati mbalimbali katika jimbo lake ,Mashuka hayo yametolewa na mfuko wa bima ya afya NHIF
Na fredy mgunda,Iringa
Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi ametoa jumla ya mashuka mia moja (100) kwenye zahanati,vituo vya afya na hospitali ya mafinga kwa lengo la kuboresha huduma za kiafya kwa wananchi wanaopata huduma katika maeneo hayo.

Akizungumza na blog hii mbunge huyo alisema kuwa aliomba mashuka kutoka mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF)kwa lengo la kuboresha huduma za kiafya katika jimbo la mafinga mjini.

“Zahanati na vituo vya afya vingi vinachangamoto nyingi lakini moja wapo ni kukosekana kwa mashuka ya kutosha kwenye maeneo mbalimbali ya kiafya hivyo nilichukua jukumu la kwenda mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF)kuomba  msaada wa mashuka na namshukuru mungu wamenisaidia na kunipa mashuka haya yote”. Alisema Chumi

Aidha Chumi aliwataka watendaji wa sekta ya afya katika jimbo la mafinga kuwahudumia wagonjwa kwa weledi wao ili kuifanya kada hiyo kuondokana na changamoto ambazo zimekuwa zikiwakumba mara kwa mara kutoka kwa wananchi.

“Nimeleta mashuka haya naomba mtumie na kuyatunza ili yaweze kudumu kwa muda mrefu kwa kuwa ni mashuka yenye ubora wa hali ya juu kama mnavyoyaona lakini boresheni huduma kwa kutoa huduma nzuri kwa wananchi hapo ndio wananchi watafurahia serikali yao”.Alisema Chumi

Chumi aliwashukuru mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF)kwa kuwapa mashuka hayo ambayo yamefanikiwa kutatua changamoto ya ukosefu wa mashuka katika jimbo la mafinga na amewaomba wazidi kuwasaidia wananchi wa jimbo hilo.

Kwa upande wao viongozi wa zahanati hizo walimshukuru mbunge wa jimbo hilo Cosato Chumi kwa kujituma na kutafuta njia za kutatua changamoto kwenye zahati zote za jimbo la Mafinga mjini tofauti na ilivyokuwa hapo awali kwa viongozi wengine.

“Unaona toka ameingia madarakani amekuwa akiwaleta viongozi mbalimbali wa serikali ili kutafuta njia za kutatua changamoto za huduma za afya,alimleta naibu waziri wa wizara ya afya na maendeleo ya jamii Hamis Kigwangala na wengine wengi kwenye sekta nyingine”. Walisema viongozi hao

Baadhi ya madiwani waliendelea kujivunia juhudi za mbunge wao kwa kazi kubwa anayoifanya kuwaletea maendeleo katika jimbo la Mafinga Mjini ambapo hapo awali ilikuwa vigumu kushudia  mbunge akijituma kama anavyofanya Cosato Chumi.

Naye mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Mafinga Charle Makoga amesema kuwa changamoto ya huduma ya afya katika vijiji vya jimbo la Mafinga ni mbaya na inahitaji juhudi binafsi kuwasaidia wananchi na kuongeza kuwa tatizo la umeme ni kubwa katika vijiji ambavyo havipokupata umeme wa REA awamu ya kwanza na pili na ndio sababu inayosababisha huduma za kiafya kudorola katika baadhi ya vijiji.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: COSATO CHUMI ATATUA TATIZO LA MASHUKA KATIKA ZAHANATI, VITUO VYA AFYA NA HOSPITALI ZA JIMBO LA MAFINGA MJINI
COSATO CHUMI ATATUA TATIZO LA MASHUKA KATIKA ZAHANATI, VITUO VYA AFYA NA HOSPITALI ZA JIMBO LA MAFINGA MJINI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhHq8smvgpSdUkToSpxWTvC-F54ZHqa_sH-du5CIw8PGdqltqsR4PBlXDYw9ma_7haYMB4MZIFdyRObNx-vtzVZSgrmAcs9e6lxXe-CWjGP15rrOMaHi_evUdweThJsTzi1cQg_6PNPN3Hi/s640/IMG_20170105_141106.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhHq8smvgpSdUkToSpxWTvC-F54ZHqa_sH-du5CIw8PGdqltqsR4PBlXDYw9ma_7haYMB4MZIFdyRObNx-vtzVZSgrmAcs9e6lxXe-CWjGP15rrOMaHi_evUdweThJsTzi1cQg_6PNPN3Hi/s72-c/IMG_20170105_141106.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/01/cosato-chumi-atatua-tatizo-la-mashuka.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/01/cosato-chumi-atatua-tatizo-la-mashuka.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy