Katibu wa Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole akifafanua mambo mbalimbali mapema leo kwenye Ofisi ndogo za Makao Makuu ya CCM, L...
Katibu
wa Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole akifafanua mambo mbalimbali
mapema leo kwenye Ofisi ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es
Salaam, kuhusiana na ushindi wa chama cha Mapinduzi (CCM) katika chaguzi
mbalimbali zilizofanyika hivi karibuni za Madiwani na nafasi ya Ubunge
huko Zanzibar.
Katika
mkutano huo na Waandishi wa Habari, alielezea siri tatu muhimu
zilizokiwezesha Chama hicho kupata ushindi, Polepole alizitaja siri ya
kwanza ni namna ya mageuzi mapya ya kimuundo na mfumo yaliyolenga
kukiwezesha CCM kurudi kwenye mikono ya wananchi kwa serikali yake
kujikita zaidi kushughulikia kero zinazowakabili Watanzania na
kufanikiwa.
Pole
Pole alisema kuwa mabadiliko hayo yamelenga kukirejesha chama wenye
misingi uliokifanya kuanzishwa kwake, akabainisha siri ya pili kuwa
ushindi huo ni matokeo ya mafanikio ya serikali katika kuweka mikakati
ya kubana mianya ya wakwepa kodi pamoja na vita dhidi ya ufisadi.
“Adui
yetu mkubwa ni rushwa na vitendo vya ufisadi nchini, Watanzania ni
mashahidi kwani muelekeo wa serikali umekuwa thabiti na tumeona
watuhumiwa wa vitendo hivyo wakichukuliwa hatua,” alisema.Alisema kuwa
siri ya tatu imetokana na kazi nzuri ya utendajikazi wa serikali kwenye
utekelezaji wa ahadi zilizotolewa na Chama.
Baadhi ya Wanahabari wakimsikiliza Ndugu Pole Pole alipozungumza nao mapema leo jijini Dar.Picha na Michuzi Jr.
Katika
hatua nyingine,Pole Pole alisema kuwa ahadi ya kutoa elimu bure kwa
wanafunzi kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha nne, imekuwa na
uhalisia mkubwa.“Na zaidi ya yote ni huduma za kiuchumi ambazo
zimeendelea kutekelezwa ambapo Chama tunaipongeza serikali na
kuikumbusha katika maeneo mengine tuliyowaahidi wananchi, ikiwemo
kuendelea kutenga asimilia 10 ya mapato ya Halmashauri kwa ajili ya
vijana na wanawake.
“Hii
itatoa nafasi kwa vijana na wanawake kupata fursa za mitaji na mikopo
yenye masharti nafuu, hivyo suala hilo linapaswa kuwekewa msisitizo
zaidi,” aliongeza.Alisema serikali inaendelea na mipango ya ujenzi wa
viwanda, vinu vya usagaji mkoani Iringa na Mwanza pamoja na kiwanda cha
mafuta ya Alizeti, mambo ambayo tayari Chama kimetoa maelekezo kwa
serikali.
Akaongeza
kuwa , ununuzi wa ndege kwa ajili ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL)
umesaidia kuwawezesha wananchi kusafiri kwenye maeneo mbalimbali katika
kufanya shughuli muhimu za kiuchumi.
Chama
Cha Mapinduzi (CCM), kimeibuka na ushindi mnene katika uchaguzi mdogo wa
marudio ya ubunge Jimbo la Diwani na udiwani kwenye kata 20 za Tanzania
Bara, Katika uchaguzi huo, kwenye jimbo la Dimani, mgombea wa CCM, Juma
Ally Juma, alipata ushindi wa kura 4,860 sawa na asilimia 78.74 dhidi
ya mpinzani wake, Abdulrazak Khatib Ramadhan wa CUF, aliyepata kura
1,234.
Ushindi
huo umedhihirisha anguko kubwa la CUF, visiwani Zanzibar kwani uchaguzi
wa mwaka 2015 licha ya kushika nafasi ya pili, kilipata wastani wa kura
2,300 lakini kwenye uchaguzi wa marudio kura zake zimeshuka kwa zaidi
ya asilimia 50.Hivyo ili kujinusuru na hali hiyo, CUF kimetakiwa
kumtafuta mchawi aliyepo ndani ya chama hicho visiwani Zanzibar na si
kulalamika.
Aidha
CCM imejizolea viti 19 vya udiwani kati ya 20 huku Chadema ikipata kiti
kimoja na kufanya Chama kudhihirisha kuwa, bado kinakubalika kwa
wananchi.Kufuatia ushindi huo, Chama kimewataka wanachama kurudisha
fadhira za ushindi huo kwa wananchi kwa kuwachagulia viongozi wenye
mioyo za kizalendo, wachapakazi waliokuwa tayari kuwasikiliza wananchi,
katika uchaguzi wa ndani unaofanyika mwaka huu.
COMMENTS