WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Dk. Frida Mokiti kubadilisha uongozi wa Kituo cha a...
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Dk. Frida Mokiti
kubadilisha uongozi wa Kituo cha afya cha Levolosi baada ya kulalamikiwa
na wananchi kuwa kinatoa huduma mbovu kwa wagonjwa hususan ni kwa wajawazito.
Pia
amewataka wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kujenga hospitali za
wilaya
ili kupunguza msongamano wa wagonjwa kwenye hospitali za rufaa.Waziri
Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Jumapili, Desemba 4, 2016) wakati
alipotembelea Hospitali ya mkoa ya Mount Meru, ambapo alisema tatizo
la msongamano wa wagonjwa hospitali za rufaa na hospitali nyingine ni
lazima lipatiwe ufunguzi.
"Hatuhitaji
kuwa na madaktari ambao wanasumbua wagonjwa. Daktari wa Mkoa hakikisha kile
kinacholalamikiwa kule Levolosi kinatafutiwa ufumbuzi. Hapa Mount Meru
hakikisheni mnaboresha mazingira ya vyoo kwenye wadi za wazazi pamoja na
kujenga sehemu ya kuoshea vyombo kwa wagonjwa, " alisema.
Awali
alipotembelea wodi ya kinamama wanaosubiri kujifungua, mmoja wa wagonjwa, Glory
Paul Mkazi wa Olasiti alimweleza Waziri Mkuu kuwa mtoto wake alifia tumboni
baada ya wauguzi na madaktari wa kituo cha Afya cha Levolosi
kuchelewa kumpatia matibabu.
"Wakati
nahudhuria kliniki nishaambiwa na daktari kuwa natakiwa kujifungua kwa njia ya
upasuaji na siwezi kujifungua kwa njia ya kawaida nilimwambia nesi kuwa
natakiwa kufanyiwa upasuaji wakanikatalia na kunilazimisha nijifungue kwa njia
ya kawaida ambapo ilishindikana na baada ya muda waliniambia kuwa mtoto amekufa
na wananifanyia upasuaji ili kuokoa maisha yangu," amesema.
.
.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Athumani Kihamia alisema amepokea
maagizo ya Waziri Mkuu, ambayo yanalenga kuboresha utoaji wa huduma bora kwa
wananchi na kusisitiza kuwa awali alichukua hatua za kinidhamu kwa watoa huduma
za afya kituoni hapo na ataendelea kusimamia nidhamu ya kazi ili kuondoa
malalamiko kwa wananchi juu ya huduma za afya.
IMETOLEWA NA:
OFISI
YA WAZIRI MKUU
JUMAPILI,
DESEMBA 4, 2016.
COMMENTS