WAZIRI MAHIGA ASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA KITAIFA YA UMOJA WA FALME ZA KIARABU

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi wa Umoja...




Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu nchini Mhe. Abdulla Ibrahim Ghanim Alsuwaidi alipowasili katika ofisi za ubalozi huo kushiriki sherehe ya madhimisho ya miaka 45 ya muungano.Tanzania na UAE zimepiga hatua kubwa za ushirikiano hususan ya kiuchumi ambapo kwa takwimu za Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) hadi Juni, 2015 makampuni 67 ya uwekezaji kutoka UAE yamewekeza hapa nchini katika sekta mbalimbali wenye thamani ya USD 497.12 Millioni na kuajiri Watanzania 9,044. Taifa la Umoja wa Falme za Kiarabu unaundwa na falme saba ambazo ni Abu Dhabi, Dubai, Sharjah, Ras Al Khaimah, Fujairah, Ajman na Umm al-Quwain.
 
 
Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Taifa la Umoja wa Falme za Kiarabu Mhe.Abdulla Ibrahim Ghanim Alsuwaidi wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka 45 ya muungano wa falme hizo.
 
 
Mhe.Waziri Balozi Dkt.Mahiga akivalishwa skafu maalum
Mhe.Waziri Balozi Dkt. Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mhe.Abdulla Ibrahim Ghanim Alsuwaidi
Wageni waalikwa wakifuatilia jambo
Balozi wa Taifa la Umoja wa Falme za Kiarabu Mhe.Abdulla Ibrahim Ghanim Alsuwaidi akizungumza wakati wa maadhimisho
Mhe. Waziri Balozi Dkt. Mahiga akitoa hutuba fupi wakati wa maadhimisho ya sherehe hizo
Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Abdalla Kilima akisalimiana na Mhe. Balozi wakati wa sherehe za maadhimisho 

----------------------------------------------------------- 

Tanzania na Umoja wa Nchi za Kiarabu (UAE) zimepiga hatua kubwa za ushirikiano hususan wa kiuchumi ambapo kwa takwimu za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) hadi Juni, 2015 Makampuni 67 kutoka UAE yamewekeza hapa nchini katika sekta mbalimbali kwa mtaji wa thamani ya Dola za Marekani milioni 497.12 na kuajiri Watanzania zaidi ya 9,044. 

Hayo yalibainishwa jana katika sherehe za kuadhimisha Siku ya Kitaifa ya UAE zilizofanyika jijini Dar Es Salaam ambapo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga alikuwa Mgeni Rasmi. 

Tanzania na UAE zinatarajiwa kufanya Mkutano wa Kwanza wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPC) ambao utakuwa chachu ya kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizi mbili hususan ya kiuchumi.

Akiongea katika hafla hiyo, Mhe. Waziri alilipongeza taifa hilo kwa kuadhimisha siku yake ya Kitaifa ikiwa imepiga hatua kubwa ya kimaendeleo ya kichumi, kijamii na kisiasa. Mhe. Waziri alisema kuwa siku hiyo ni inatoa fursa pia ya kutathmini mahusiano mazuri yaliyopo baina ya Tanzania na UAE. 

Kwa upande wake, Balozi wa UAE hapa nchini, Mhe. Abdulla Ibrahim Ghanim Alsuwaidi aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mkubwa inayotoa kwa Ubalozi huo ambao unamwezesha kutekeleza majukumu yake kwa wepesi ikiwa ni pamoja na kuimarisha mahusiano ya nchi hizi mbili. Mhe. Balozi aliahidi kuendeleza ushirikiano huo hususan katika kutimiza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda. 

Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) unajumusha falme saba ambazo ni Abu Dhabi, Dubai, Sharjah, Ras Al Khaimah, Fujairah, Ajman na Umm al-Quwain huadhimisha siku yake ya Kitaifa tarehe 02 Disemba ya kila mwaka tokea mwaka 1971.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI MAHIGA ASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA KITAIFA YA UMOJA WA FALME ZA KIARABU
WAZIRI MAHIGA ASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA KITAIFA YA UMOJA WA FALME ZA KIARABU
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEghTAnL0AVirbzSCccPLfMBShfBW2jI2R3V5brgXEeZkWA_FdJSl233xIeDmef6eqLQZOAoURUcmgYxEzs2NTk_hKyPbaDN4mc7GYFACv61BhHd2RIWFUhpP39obMvgYIF72YXDiB4quz8/s640/719A4788.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEghTAnL0AVirbzSCccPLfMBShfBW2jI2R3V5brgXEeZkWA_FdJSl233xIeDmef6eqLQZOAoURUcmgYxEzs2NTk_hKyPbaDN4mc7GYFACv61BhHd2RIWFUhpP39obMvgYIF72YXDiB4quz8/s72-c/719A4788.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/12/waziri-mahiga-ashiriki-maadhimisho-ya.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/12/waziri-mahiga-ashiriki-maadhimisho-ya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy