WANAWAKE WAONGOZA KUWA NA VVU NCHINI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na...





Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam kuhusu siku ya UKIMWI Duniani. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Dk. Hamis Mwinyimvua. 
 
 

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko akifafanua juu ya takwimu za maambukizi ya UKIMWI wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama.

 
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO

Utafiti wa Viashiria vya Virusi vya UKIMWI (VVU) na Maralia (THMIS) wa mwaka 2011/2012 kwa upande wa Tanzania Bara vinaonyesha kuwa idadi kubwa ya wanawake wameambukizwa ugonjwa huo kuliko wanaume.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama alisema takwimu zilizopo sasa zinaonyesha kuwa asilimia 6.2 ya wanawake wameambukizwa ugonjwa wa ukimwi ikilinganisha na asilimia 3.8 ya wanaume.

Waziri Mhagama alisema kuwa kutokana na utafiti huo, maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa upande wa Tanzania Bara ni asilimia 5.3 na inakadiriwa  kuwa  jumla ya watanzania 1,538,382 wanaishi na VVU ambapo vijana wenye umri kati ya 15-24 ni asilimia 10.6 na watoto walio chini ya miaka 15 ni 11.8.

“UKIMWI bado ni janga kubwa nchini Tanzania kwani takwimu zinaonyesha kuwa  maambukizo mapya yanakadiriwa kufikia watu 48,000 kwa mwaka hali ambayo  inaashiria kupoteza  nguvu kazi kubwa katika nchi yetu”

Kwa mujibu wa Waziri Mhagama alisema Tanzania itendelea kushirikiana na nchi nyingine Duniani kuhakikisha wanatokomeza janga la ugonjwa huo  ifikapo mwaka 2030.

Aliongeza kuwa Serikali inaendelea kuwahamisha wananchi waendelee kujitokeza kupima afya zao ili wajitambue na kujua namna ya kujilinda kwani Shirika la Afya Duniani (WHO) linasisitiza nchi wanachama kuwaanzishia dawa mara moja watu wote watakaopima na kugundulika kuwa na VVU.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko alisema kuwa kwa mwaka 2015 walioambukizwa VVU walikuwa Watanzania 2,100,000 ambayo ni idadi kubwa ukilinganisha na idadi ya sasa lakini  pamoja na kushuka kwa idadi hiyo wananchi wanatakiwa kuendelea kujilinda mara dufu.

”Ingawa maambukizi ya VVU yameshuka kutoka Watanzania 2,100,000 hadi 1,538,382, Watanzania hatutakiwi kubweteka bali tunatakiwa tufanye jitihada za pamoja kuhakikisha janga hili linafikia mwisho,”alisema Dk. Maboko.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WANAWAKE WAONGOZA KUWA NA VVU NCHINI
WANAWAKE WAONGOZA KUWA NA VVU NCHINI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEitQ4maf0a89Hosqs5eBPGGoypCit7mRuL2S7Y_sq1k602Bcg1L3yccZWhuYmaroEzIWlNEqQ7w2vPlBRvkF87CfYYLE9njXmwFTU3S4L0Ov7X-BGqfDkL2lCMNfB3CLSRu01z_r-NAQxU/s640/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEitQ4maf0a89Hosqs5eBPGGoypCit7mRuL2S7Y_sq1k602Bcg1L3yccZWhuYmaroEzIWlNEqQ7w2vPlBRvkF87CfYYLE9njXmwFTU3S4L0Ov7X-BGqfDkL2lCMNfB3CLSRu01z_r-NAQxU/s72-c/1.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/12/wanawake-waongoza-kuwa-na-vvu-nchini.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/12/wanawake-waongoza-kuwa-na-vvu-nchini.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy