TAFITI: MALARIA BADO NI GONJWA LINAOENDELEA KUUA WATOTO WA CHINI YA MWAKA MMOJA KWA WINGI NCHINI

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiongea na wadau mbalimbali katika uzinduzi wa...




Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiongea na wadau mbalimbali katika uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es Salaam leo.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akizindua Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es Salaam leo.
 
 
 Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akiongea na  wadau mbalimbali katika Uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es Salaam leo.
 
 
 Meneja wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Sylivia Meku akielezea kwa wadau wa afya Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es Salaam leo.
 
 
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa kabla ya uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Kaimu Katibu Mkuu  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mohamed Ally.
 
 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja wadau mbalimbali wa Takwimu na Afya katika uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Benjamin Sawe- Maelezo)

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Waziri wa Afya na Maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto, Ummy Mwalimu, amesema kuwa Utafiti unasema kuwa kiwango cha maambukizi ya Malaria kwa watoto chini ya mwaka mmoja kuwa malaria bado ni mojawapo ya magonjwa yanayoongoza kwa kusababisha vifo vya watoto Nchini.

Ummy amesema hayo jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa taarifa ya utafiti wa afya ya uzazi na mtoto na Malaria Tanzania ya mwaka 2015-16 (TDHS-MIS), katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.

“ asilimia kubwa ya vifo vya watoto na akina mama wajawazito. Kiwango cha maambukizi ya malaria kwa watoto chini ya mwaka mmoja kimeongezeka kutoka asilimia 14 mwaka 2015/16 ukilinganisha na asilimia (9) ya mwaka 2010 kwa kutumia kipimo cha kutoa matokeo kwa haraka yaani Rapid Diagnostic Tests (RDT)” amesema Waziri Ummy.

Ameongeza kuwa anatambua kwamba, suala hili limeshaanza kufanyiwa kazi ndani ya Wizara na niwaombe wadau wote tushirikiane kwa pamoja katika kuendeleza juhudi zilizopo za kuhakikisha Malaria inamalizwa hapa Tanzania. Hivyo natambua Mpango wa Kudhibiti Malaria Tanzania (NMCP) upo katika utekelezaji wa awamu nyingine ya kusambaza vyandarua katika Kaya za Tanzania, tunategemea juhudi hizi na nyingine zinazofanywa na wadau wengine zitachangia kupunguza kiwango cha Malaria hapa nchini.

Katika hatua nyingine Waziri Ummy ameweza kuzungumzia tatizo la Mimba za utoto kwa watoto wa kike walio na miaka 15 hadi 19 na kusema kuwa matokeo yanaonesha kuwa asilimia 27 ya wasichana wenye umri wa miaka 15 hadi 19 wa mwaka 2015/16 wameshaanza kuzaa kulinganisha na asilimia 23 ya mwaka 2010.

Ameongeza kuwa bado hii ni changamoto ambayo sote kwa pamoja tunatakiwa kukabiliana nayo kwa kutoa elimu zaidi ili kupunguza kiwango hiki na kuwezesha watoto wa kike waweze kupata muda wa kusoma na kujiendeleza katika kujiandaa na maisha yao ya baadae. Hivyo, Serikali itaendelea kutoa elimu juu ya madhara yanayoweza kutokea kwa wasichana kuzaa wakiwa bado wadogo

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TAFITI: MALARIA BADO NI GONJWA LINAOENDELEA KUUA WATOTO WA CHINI YA MWAKA MMOJA KWA WINGI NCHINI
TAFITI: MALARIA BADO NI GONJWA LINAOENDELEA KUUA WATOTO WA CHINI YA MWAKA MMOJA KWA WINGI NCHINI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgD6_cNYm4VVF4y364HQPLgll2cCdKBTndihx-HI-8dRlbpCO8U9vXLOPfXiLRukfZNzwT0FhRPYjBWgTcjx8DFe5fuDIVgD8d51B9qSvuP3HhQxe3HKUg-_qmehbx_XELNgJB6eHQHG-8T/s640/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgD6_cNYm4VVF4y364HQPLgll2cCdKBTndihx-HI-8dRlbpCO8U9vXLOPfXiLRukfZNzwT0FhRPYjBWgTcjx8DFe5fuDIVgD8d51B9qSvuP3HhQxe3HKUg-_qmehbx_XELNgJB6eHQHG-8T/s72-c/1.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/12/tafiti-malaria-bado-ni-gonjwa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/12/tafiti-malaria-bado-ni-gonjwa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy