SIKU YA PILI YA SAFARI YA WANAHABARI NA ASKARI WA JESHI LA ULINZI KUELEKEA KILELE CH UHURU, MLIMA KILIMANJARO
HomeJamii

SIKU YA PILI YA SAFARI YA WANAHABARI NA ASKARI WA JESHI LA ULINZI KUELEKEA KILELE CH UHURU, MLIMA KILIMANJARO

Baada ya mapumzko ya siku ya kwanza katika kituo cha Mandara,timu ya Wanahabari na Asakari wa jeshi la Ulinzi asubuhi yake walip...

DKT. SHEIN AWAONGOZA VIONGOZI MBALIMBALI KATIKA HITMA YA RAIS WA KWANZA WA ZANZIBAR MZEE ABEID KARUME MJINI UNGUJA
TRA INAUNGANA NA WATANZANIA WOTE KATIKA KUMBUKUMBU YA RAIS WA KWANZA WA ZANZIBAR MHE. SHEIKH ABEID AMANI KARUME
TANESCO YAKABIDHI MRADI WA UMEME KWENYE SHULE YA MSINGI GARAGAZA HUKO KIBAHA











Safari ilianza  kwa kila mshiriki kuoenkana mwenye afya na nguvu ya kufikia ndoto ya kufika kilele cha Uhuru.


Baada ya kupita katika msitu mnene wakati wa kuanza safari uelekeo wa kituo cha Mandara na baadae kutoka Mandara kuelekea Horombo,kidogo kidogo hali ya uoto ilionekana kubadilika kadri washiriki walivyokuwa wakielekea sehemu za juu. 

Mwendo wa takribani saa saba kuanzia majira ya saa 2:30 asubuhi  kutokea Mandara.Washiriki wakafika eneo la nusu njia kuelekea Horombo na kupata chakula cha Mchana.

Safari ikaendelea.
Hatimaye majira ya saa 11 jioni ,timu ya Wanahabari na Askari wa jeshi la Ulinzi wakaingia katika kituo cha Horombo.
Kama ilivy ada kuchukua kumbukumbu likawa jambo la muhimu kwao ,na hapa wakapa picha ya pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu na Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi TANAPA,Jenerali George Waitara  aliyekuwa mkuu wa msafara.
Majira ya usiku wa saa moja ,timu ilipata chakula cha usiku na maelekezo kutoka kwa mkuu wa waongoza watalii ,Chombo kwa ajili ya siku iliyofuata.
Siku iliyofuata ilikua ni siku ya mazoezi ,siku hii ilitengwa kwa ajili ya kuzoea hali ya hewa ya juu wenyewe wanaita "Climatization",mazoezi yalikuwa ni kufanya safari ya kueleke eneo lijulikanalo kama Zebra.
Safari ya kuelekea Zebra ikaanza.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu ,Jenerali George Waitara pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii ,Mstaafu ,Balozi Charles Sanga pia walikuwa katika safari hiyo ya mazoezi.
Hatimaye timu ikafika eneo la Zebra.
Baadahi yao Washiriki wakapata nafasi ya kupata kumbukumbu na wageni kutoka Japan walikuwa wakipanda mlima Kilimanjaro kama Watalii.
Timu ikapata picha ya pamoja na Naibu Kamanda wa kikosi cha Ardhini,Brigedia Jenerali ,Jairo Mwaseba baada ya kufika katika eneo la Zebra.
Eneo la Zebra umaarufu wake unatokana na michoro iliyopo katika Mawe makubwa ikiwa mithili ya pundamilia.
Majira ya jioni baada ya kurudi kituo cha Mandari, timu ilijiandaa na safari ya kuekeea kituo cha Kibo,hali ya hewa eeo hili ilikuwa ni ya kubadilika badilika kila mara zaidi baridi ikiambatana na ukungu ndio ilitawala.

(Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii aliyekuwa katika safari hiyo)


Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: SIKU YA PILI YA SAFARI YA WANAHABARI NA ASKARI WA JESHI LA ULINZI KUELEKEA KILELE CH UHURU, MLIMA KILIMANJARO
SIKU YA PILI YA SAFARI YA WANAHABARI NA ASKARI WA JESHI LA ULINZI KUELEKEA KILELE CH UHURU, MLIMA KILIMANJARO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhRnSNYlspp3ThuptVY764UUxJ0TEkt0AZsu9011rPxot7_D_YU4KGVaDDN0xBPsiyonGAa7Vx2bp9UsikXEHVbn_ljLOcD5p8IY0NRRwCXbSzlG7X2tY4Qn2GA_Zbp1nWf-0wwx9kNNQ3x/s640/_MG_0012.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhRnSNYlspp3ThuptVY764UUxJ0TEkt0AZsu9011rPxot7_D_YU4KGVaDDN0xBPsiyonGAa7Vx2bp9UsikXEHVbn_ljLOcD5p8IY0NRRwCXbSzlG7X2tY4Qn2GA_Zbp1nWf-0wwx9kNNQ3x/s72-c/_MG_0012.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/12/siku-ya-pili-ya-safari-ya-wanahabari-na.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/12/siku-ya-pili-ya-safari-ya-wanahabari-na.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy