Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt. Ali Mohamed Shein akikata Utepe ikiwa ni ishara ya ufunguz...
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt. Ali Mohamed Shein
akikata Utepe ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa Msikiti,
Masjid Muhammad (S.A.W) uliojengwa na Kampuni ya Al-Buwardy
huko Fujoni Mzambarauni Wilaya ya Kaskazini B" Mkoa wa Kaskazini Unguja Desemba 30, 2016. Wanaoshuhudia ni, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja
Mhe,Vuai Mwinyi Mohamed na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi
wa Umma na Utawala Bora Mhe Haroun Ali Suleiman (kushoto). (PICHA NA IKULU YA
ZANZIBAR).
Rais akifunua kitambaa kuzindua msikiti huo.
Rais, akipokelewa wakati akiwasili kwenye ufunguzi huo.
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt. Ali Mohamed Shein
(kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe,Vuai Mwinyi
Mohamed wakati alipowasili katika ufunguzi wa msikiti, Masjid Muhammad (S.A.W)
huko Fujoni Mzambarauni Wilaya ya Kaskazini B" Mkoa wa kaskazini Unguja Desemba 30, 2016. Msikiti huo umejengwa chini ya usimamizi wa Bw,Yakoub
Othman mwakilishi wa Kampuni ya Al-Buwardy Tanzania.
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein
(kulia) akisalimiana na Bw. Samir Ayoub mmoja wa wanafamilia ya Yakoub Othman,
msimamizi wa ujenzi wa msikiti huo.
Sheikh
Otman Maalim alipokuwa akitoa mawaidha baada ya ufunguzi wa Msikiti
Masjid Muhammad (S.A.W).
Rais akihutubia waumini baada ya ufunguzi huo
Waumini waliohudhuria sherehe za ufunguzi wa msikiti huo.
Ni wakati wa sala
COMMENTS