MBUNGE KABATI KUKARABATI SHULE YA MSINGI AZIMIO SIKU YA IJUMAA HII

  Mwenyekiti wa  chama cha mapinduzi (CCM) wilaya  ya iringa Abeid Kiponza,mbunge wa viti maalumu mkoani ...


 

Mwenyekiti wa  chama cha mapinduzi (CCM) wilaya  ya iringa Abeid Kiponza,mbunge wa viti maalumu mkoani iringa  kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela wakiwa katika moja ya madarasa ya shule ya msingi Azimio wakati wa kujadili jinsi gani ya kutatua changamoto za shule hiyo.
 
 
Mbunge wa viti maalumu mkoani Iringa  kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akikagua miundombinu ya shule ya msingi Azimio sambamba na wananchi na viongozi wa shule hiyo.
 
 
Hili ni moja kati ya madarasa ya shule ya msingi Azimio ambalo lipo taabani kabisa na likiwa linakaribia kuanguka kutokana na kuwa na nyufa nyingi ambazo ni kubwa sana.
 
Hili ni moja kati ya  madarasa ya shule ya msingi Azimio ambao linaonekana afadhari kidogo na kuwashawishi viongozi mbalimbali kuketi na kujadili maswala ya kutatua changamoto za shule hiyo ambapo madarasa mengine yapo taabani kuliko hili.

Na Fredy Mgunda, Iringa

Mbunge wa viti maalum mkoani Iringa Ritta Kabati anatarajia kukarabati shule ya msingi ya Azimio iliyopo manispaa ya Iringa kutokana na uchakavu wa majengo hayo.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa miundombinu ya shule hiyo mbunge Kabati alisema ni aibu kwa shule kongwe kama hiyo  kuwa miundombinu mibovu kama hiii.

Kabati aliongeza kuwa shule hiyo imeharika hovyo na inahitaji msaada wa haraka kuikarabati kwa kuwa wananfunzi wanasoma katika mazingira magumu na kudumisha elimu ya wanafunzi hao.

“Hii shule imeanza sawa na siku niliyozaliwa mimi lakini ukiiangalia imechakaa na imechoka hivyo sina budi kuanza kuikarabati shule hii kwa kuwa ni aibu kwangu haiwezakani shule ikawa manispaa ya iringa halafu ikawa katika muundo huuu”alisema kabati

Aidha Kabati alisema kuwa hadi kufikia siku ya ijumaa ya tarehe 23 mwezi wa kumi na mbili atahakikisha anakarabati shule yote ili iwe  katika ubora unaotakiwa kama shule nyingine zilizopo manispaa ya iringa.

“Tunashule bora sana hapa manispaa ya iringa lakini hii ya Azimio imekuwa katika hali mbaya sana ni jukumu langu kama mbunge wa mkoa wa iringa kutatua changamoto mbalimbali zinazoukabili mkoa wangu”alisema Kabati

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alisema haiwezekani shule ya azimio ikawa katika mazingira mabovu ya miundombinu kama yale hiyo hadi kufikia siku ya ijumaa atahakikisha anakarabati  shule hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

Naye mkuu wa shule ya msingi Willfrid Chotipembe alimshukuru mbunge wa viti maalum Ritta Kabati pamoja na mkuu wa wilaya kwa kufika shuleni hapo na kuahidi kutatua changamoto zinazoikabili shule hiyo.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MBUNGE KABATI KUKARABATI SHULE YA MSINGI AZIMIO SIKU YA IJUMAA HII
MBUNGE KABATI KUKARABATI SHULE YA MSINGI AZIMIO SIKU YA IJUMAA HII
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhIofLWYrdW-CRwW0SXu_QUg7aqSa9GTI3ahdPSs6jg_lIboQKeKKYmDAyKp9jFA77zCYtrprChN7gUFzUzlfKNJ3N7qdvSq1djuqgVZbzrhUw3fUL0EwY5NbJBqGsFV_rwkrg2W3sWOEBa/s640/IMG_20161221_140043.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhIofLWYrdW-CRwW0SXu_QUg7aqSa9GTI3ahdPSs6jg_lIboQKeKKYmDAyKp9jFA77zCYtrprChN7gUFzUzlfKNJ3N7qdvSq1djuqgVZbzrhUw3fUL0EwY5NbJBqGsFV_rwkrg2W3sWOEBa/s72-c/IMG_20161221_140043.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/12/mbunge-kabati-kukarabati-shule-ya.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/12/mbunge-kabati-kukarabati-shule-ya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy