MASAUNI KUYAFUTA MASHIRIKA YANAYOBARIKI USHOGA NCHINI, AWATAKA VIJANA KUISHI KWA KUFUATA MAADILI MEMA YA DINI
HomeJamii

MASAUNI KUYAFUTA MASHIRIKA YANAYOBARIKI USHOGA NCHINI, AWATAKA VIJANA KUISHI KWA KUFUATA MAADILI MEMA YA DINI

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa koti) akiwasili katika Ziara ya Shekhe Uwesu bin Muham...

NEWS ALERT; KIGWANGALLA AAGIZA MSAKO MKALI KWA WALIOUA SIMBA TISA SERENGETI
VIDEO- MAKAMU WA RAIS AZINDUA UKUTA WA FUKWE WA BAHARI- BARABARA YA BARACK OBAMA DAR ES SALAAM
RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA MAJAJI WATATU IKULU JIJINI DAR ES SALAAM



Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa koti) akiwasili katika Ziara ya Shekhe Uwesu bin Muhammad Alqadiriya iliyofanyika katika Zawiya ya Shekhe Mahadh Kigamboni,  jijini Dar es Salaam jana. Katika hotuba yake Masauni aliwataka vijana kuwa makini na mashirika ambayo yanahamasisha ushoga nchini na pia alitangaza kuyafuta mashirika hayo endapo yakigundulika. 
 
NA FELIX MWAGARA (MOHA)
NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amewataka vijana nchi kuwa makini na baadhi ya Mashirika yasiyokuwa ya Serikali ambayo yanajishughulisha na uhamasishaji wa mapenzi ya jinsia moja (ushoga).
Mhandisi Masauni alisema, Mashirika hayo hayapaswi kuwepo nchini kwani yanafanya kazi kinyume na mila na desturi ya nchi yetu na yanapaswa kufutwa haraka iwezekanavyo endapo yatagundulika.
Akizungumza katika Ziara ya Shekhe Uwesu bin Muhammad Alqadiriya iliyofanyika katika Zawiya ya Shekhe Mahadh Kigamboni,  jijini Dar es Salaam, Mhandisi Masauni aliongeza kuwa, vijana wanapaswa wawe makini katika maisha yao, kamwe wasikubali kupotoshwa pamoja na kuendeshwa na kundi lolote ambalo linafanya kazi kinyume na taratibu za nchi.
“Kuna baadhi ya mashirika ambayo yanajihusisha kwa kutoa elimu na kuhamasisha ndoa za jinsia moja, mashirika hayo yanafanya kazi kinyume na sheria ya nchi, hivyo tunayachunguza na tukiyagundua hakuna cha Mswalie Mtume, tutayafuta haraka iwezekanavyo,” alisema Masauni.
Pia aliwataka Watanzania kutoa taarifa ya uwepo ya taasisi hizo binafsi zinazofanya shughuli hizo nchini muda wowote wakizigundua ili zifuatiliwe kwa umakini na hatimaye zifutwe haraka iwezekanavyo kwa kuwa zinaharibu jina zuri la Tanzania.
Masauni ambaye alikuwa na Kadhi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shekhe Hamid Masoud Jongo katika sherehe hiyo, licha ya kuwashukuru waandaaji wa tukio hilo kwa kumualika, pia aliwahasa Waislam nchini wawe na umoja, wapendane na waache kulalamika kwa kuwa mafundisho ya dini hiyo yanaelekeza mambo mema ambayo kila Muislam anatakiwa kuyafuata.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia aliyekaa) akimsikiliza Kadhi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shekhe Hamid Masoud Jongo alipokuwa akizungumza na Waislam katika Ziara ya Shekhe Uwesu bin Muhammad Alqadiriya iliyofanyika katika Zawiya ya Shekhe Mahadh Kigamboni, jijini Dar es Salaam leo. Mgeni rasmi katika sherehe hiyo, Mhandisi Masauni, katika hotuba yake aliwataka vijana kuwa makini na mashirika ambayo yanahamasisha ushoga nchini, na pia alitangaza kuyafuta mashirika hayo endapo yakigundulika
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia aliyekaa) na  Kadhi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shekhe Hamid Masoud Jongo (wapili kulia waliokaa) wakimsikiliza Shekhe wa Wilaya ya Kigamboni, Abdalla Idd alipokuwa akizungumza na Waislam katika Ziara ya Shekhe Uwesu bin Muhammad Alqadiriya iliyofanyika katika Zawiya ya Shekhe Mahadh Kigamboni, jijini Dar es Salaam leo. Mgeni rasmi katika sherehe hiyo, Mhandisi Masauni, katika hotuba yake aliwataka vijana kuwa makini na mashirika ambayo yanahamasisha ushoga nchini, na pia alitangaza kuyafuta mashirika hayo endapo yakigundulika
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MASAUNI KUYAFUTA MASHIRIKA YANAYOBARIKI USHOGA NCHINI, AWATAKA VIJANA KUISHI KWA KUFUATA MAADILI MEMA YA DINI
MASAUNI KUYAFUTA MASHIRIKA YANAYOBARIKI USHOGA NCHINI, AWATAKA VIJANA KUISHI KWA KUFUATA MAADILI MEMA YA DINI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhrM0gL84KVsJ7EoR78IpnkDgHdjKbAqxsvF28DnFQ3CB6GVxgxP731gYVEx3yeCI81hDQwXPt0ytSR7oTbdr6sxqsEVuzvd-2jpmg5i1cp4s01cpOK8Aq4JlKZMcItg6ispAL93w4iABw/s640/PIX+1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhrM0gL84KVsJ7EoR78IpnkDgHdjKbAqxsvF28DnFQ3CB6GVxgxP731gYVEx3yeCI81hDQwXPt0ytSR7oTbdr6sxqsEVuzvd-2jpmg5i1cp4s01cpOK8Aq4JlKZMcItg6ispAL93w4iABw/s72-c/PIX+1.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/12/masauni-kuyafuta-mashirika-yanayobariki.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/12/masauni-kuyafuta-mashirika-yanayobariki.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy