Ismail Khalfan Mrisho, mchezaji wa timu ya vijana ya Mbao FC ya jijini Mwanza, akishangilia bao alilofunga kwa kisigino kwa ...
 |
Ismail Khalfan Mrisho,
mchezaji wa timu ya vijana ya Mbao FC ya jijini Mwanza, akishangilia
bao alilofunga kwa kisigino kwa style ya nyoka, muda mfupi kabla ya
kufariki Dunia, wakati wa pambano lake dhidi ya Mwadui ya Shinyanga.
Uchunguzi wa madaktari wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kagera, umebaini
kuwa mchezaji huyo alifariki baada ya moyo wake kusimama ghafla kufanya
kazi, na tayari mazishi yake yamefanyika leo Desemba 5, 2016 nyumbani
kwao Mabatini jijini Mwanza. |
Mshambuliaji wa timu ya vijana ya Mbao Fc U-20 Ismail Mrisho Khalfan
anayevalia jezi nambari 4 amefariki Dunia jioni hii baada ya kuanguka
Uwanjani Kaitaba wakati wa Mtanange wao dhidi ya timu ya vijana wa
Mwadui ikiwa ni mechi ya mwisho ya kumaliza duru la kwanza la ligi ya
Vijana. Ismail Mrisho Khalfan amefariki akiwa na miaka 19.
Ismail Mrisho Khalfan akipata huduma ya kwanza kutoka kwa madaktari wa Timu yake leo hii kwenye Uwanja wa Kaitaba.
Akipata Huduma ya haraka baada ya kuanguka Uwanjani. Picha na Faustine Ruta, Bukoba

Mshambuliaji wa timu ya vijana ya Mbao Fc U20 Ismail Mrisho Khalfan
anayevalia jezi nambari 4 amefariki Dunia jioni hii baada ya kuanguka
Uwanjani Kaitaba wakati wa Mtanange wao dhidi ya timu ya vijana wa
Mwadui ikiwa ni mechi ya mwisho ya kumaliza duru la kwanza la ligi ya
Vijana.
Ismail Khalfan amefariki akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mjini Bukoba.
Ismail Mrisho Halfan alifariki akiwa njiani kuelekea Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Kagera iliyoko katika Manispaa ya Bukoba.

Mrisho Halfan ndie aliyeifungia bao la kwanza na bao la pili lilifungwa kwa mkwaju wa Penati hivyo mtanange kumalizika kwa 2-0.
ISMAIL
MRISHO HALFAN watatu kutoka kushoto, muda mfupi kabla ya Mtanange wao
kuanza leo kwenye Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba. Picha zote na Faustine
Ruta.
Ismail Khalfan kabla ya kufikiwa na umauti aliweza kuifungia
timu yake bao la kwanza na bao la pili lilifungwa kwa mkwaju wa Penati
hivyo mtanange kumalizika kwa 2-0.
Kabla ya kuanguka Ismail
aligongana na beki wa Mwadui Fc na baadae akiwa peke yake alianguka
chini lakini akainuka halafu akaanguka tena na kutokana na ukosefu wa
huduma ya kwanza na gari la wagonjwa Katika Uwanja wa Kaitaba
kulipelekea marehemu kupandishwa kwenye gari la zima moto na kupelekwa
hospital ambapo mauti yalimkuta.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.





Mchezaji
Ismail Mrisho Halfan wa timu ya Mbao U-20 akitolewa uwanjani na watu
wa msalaba Mwekundu baada ya kuanguka uwanjani wakati wa mchezo wao
uliokuwa ukichezwa katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba
Mchezajiwa Mbao U- 20, Ismail Mrisho Halfan akipandishwa
kwenye gari la Zimamoto baada ya kutokuwepo gari la kubebea wagonjwa
kwenye uwanja Kaitaba mjini Bukoba
Gari
la zimamoto klikiondoka uwanjani Kaitaba ikiwa imebeba mchezaji Ismail
kuelekea hospitali ya Mkoa wa Kagera. (Picha na Faustine Ruta)
Hivi ndivyo mtanange ulivyokuwa Uwanjani Kaitaba jioni hii.
Shangwe!
Ismail Mrisho Khalfan(kulia)
Ismail Mrisho Khalfan(kulia) akitupia shangwe kwenye Camera yetu
Vijana wa Mbao Fc walianza kipindi cha kwanza wakiwa kwenye hali ya kutaka kuibuka na ushindi
Ismail Mrisho Khalfan(kulia) akimkacha mchezaji wa Mwadui fc
COMMENTS