hawa ni baadhi ya wananchi wa kabila la kimasai ambalo linakaliwa na tuhuma za kuozesha wasicha wenye umri mdogo. ...
hawa ni baadhi ya wananchi wa kabila la kimasai ambalo linakaliwa na tuhuma za kuozesha wasicha wenye umri mdogo.
hili ni jengo la shirika lisilo la kiserikali la Ilula Ophan program (IOP)
Na Fredy Mgunda, Iringa
Shirika
lisilo la kiserikali la Ilula Ophan program (IOP) limeendelea kukemea
na kutoa elimu juu ya ndoa za utotoni kwa kuwa zinarudisha maendeleo
nyuma ya wasichana wa jamii ya kimasai.
Akizungumza
na blog hii Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Ilula Ophan
program (IOP) Edson Msigwa alisema kuwa tatizo la ndoa za utotoni katika
kabila la wamasai bado ni kubwa.
Msigwa alieleza jinsi gani wanavyofanya shughuli za kukemea na kutoa elimu juu ya ndoa za utotoni katika jamii ya wamasai
“Tunajitahidi
kuwafikia jamii zote za wilaya ya kilolo mkoani iringa kwa lengo la
kutoa elimu lakini tunakumbana na changamoto kutoka kwa wazazi ambao
bado wana mila potofu hasa huku umasaini”alisema Msigwa
Aidha Msigwa alisema kuwa kila siku ndoa za utotoni zinaongezeka huko vijijini na kuitaka serikali kukubali takwimu wanazozitoa kwa kuwa zinaukweli.
“Sisi
hapa Ilula Ophan program (IOP) tunaishi na wasichana wa kabila la
kimasai wafanikiwa kukimbia kuozeshwa wakiwa na umri mdogo hebu
mwangalie huyo motto joyce alivyo alitakiwa aolewe na umri huu wa miaka
kumi nan ne je unafikiri ni haki jamiii inatakiwa kubadili na serikali
inatakiwa kuongeza juhudi kulitatua hili”alisema Msigwa
Naye
mmoja wa wasichana wa kimasai aliyekimbia kuolewa akiwa na umri mdogo
Joyce Hassani alisema kuwa msichana wa kimasai wakimaliza elimu ya
msingi wanalazimishwa kuolewa na familia yake.
“Mimi
na mwenzangu tumemaliza shule tu wametupeleka kucheza ngoma kisha
kutaka kutuozesha lakini mungu mwema tulifanikiwa kukimbia na kufika
hapa Ilula Ophan program (IOP) japo kuwa wanaume wa kimasi wanakuja hapa
kituoni mara kwa mara kutaka kutuiba turudi kule umasaini ili tukaolewe
hasa kaka zangu”alisema joyce
Joyce
ameiomba serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali kusaidia kupambana
na mila potofu zinazowapotezea malengo wasichana wa kimasai.
“Angalia
tunavyoteseka saizi tunaishi kama watoto yatima wakati wazazi wetu wapo
na wana afya zuri kabisa lakini tatizo kubwa sisi wasichana wadogo wa
kimasai tunaolewa tukiwa na umri mdogo sana tunaomba jamii iamuke na
kutusaidia kutatua tatizo hilo.”alisema Joyce
Zipo
sababu nyingi na ushahidi mwingi wa kisayansi, unaonyesha kuwa, ndoa na
mimba katika umri mdogo ni hatari kwa afya na mstakabali wa maisha yake
na mtoto wake.
Wasichana wanaopata ujauzito na kujifungua katika umri mdogo wengi wao pia hupata tatizo la fisitula - Vescovaginal fistula.
Kwa
mujibu wa utafiti uliofanywa na chama cha waandishi wahabari wanawake
(TAMWA) umeonesha kuwa katika mwaka 2012-2013 matukio 228 ya mimba na
matukio 42 ya ndoa za utotoni yaliripotiwa nchini tanzania.
COMMENTS