GARI LA MBUNGE WA MBEYA MJINI (SUGU) LAGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO

  Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (SUGU) Na JamiiMojaBlog, Mbeya Mkazi wa Iyunga jijini Mbeya ambaye ame...


 







Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (SUGU)


Na JamiiMojaBlog, Mbeya
Mkazi wa Iyunga jijini Mbeya ambaye amefahamika kwa jina moja la Rechal (13) amefariki dunia mara baada ya kugongwa na gari , namba T161 CPP Toyota LandCruiser inayodaiwa kumilikiwa na Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi maharufu kwa jina la (SUGU), kwenye kivuko cha barabara (ZEBRA) na kumsababishia kifo chake papo hapo.
Tukio hilo limetokea leo Desemba 17  majira ya saa mbili asubuhi huko katika eneo la Iyunga Jijini hapa, wakati gari ya Mbunge huyo ikiwa njiani kuelekea uwanja wa ndege wa Songwe kwa ajili ya mapokezi ya kiongozi wa Kitaifa Freeman Mbowe.
Imeelezwa kuwa, gari hilo likiwa katika mwendokasi linadaiwa kukiuka sheria za barabarani kwa kutosimama kwenye kivuko cha barabara kinachowaruhusu watembea kwa miguu kuvuka na kumgonga mtoto huyo  na kusababisha kifo chake papo hapo.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wakizungumza , kwa nyakati tofauti , wamesema mtoto huyo akiwa na mama yake walikuwa wakivuka barabara baada ya magari ya upande wa  pili kusimama na kuwaruhusu watembea kwa miguu hao kuvuka.
Amesema, wakiwa katikati ya kivuko hicho mama wa marehemu alishangaa kuliona gari ya Mbunge hiyo ikija kwa kasi hivyo kumuachia mtoto wake aliyekuwa amemshika mkono na yeye kutafuta njia ya kujiokoa.
Wameeleza kuwa  licha ya dereva wa gari ya Mbunge kuona madereva wenzie wa magari yaliyokuwa yakitokea Mbalizi wakisimama kwa ajili ya kuwaruhusu watembea hao kuvuka lakini yeye akitokea mjini Mbeya alishindwa kutii sheria hiyo na kupita akiwa katika mwendo kasi.
“Madereva wenzie tumesimama ili mama na mtoto wavuke lakini yeye akiwa na haraka alipita tu, kwa kweli hii inauma sana, nasikia mtoto amepoteza maisha lakini mama amejeruhiwa na kwamba amekimbizwa hospitali Teule ya Ifisi kwa matibabu,”alisema mmoja wa mashuhuda hao.

Gari la Mbunge wa Mbeya mjini Mheshimiwa Joseph Mbilinyi (Sugu) Toyota Land Cruser T.161 CPP likiwa ofisi za Usalama barabarani jijini Mbeya baada ya kugonga mtembea kwa miguu na kusababisha kifo .

Kamanda wa  Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari akizungumza kwa njia ya simu amekiri kutokea kwa tukio hilo na kuthibitisha kifo cha mtoto huyo.
 Aidha Kivadashari ametaja jina la dereva wa gari hiyo kuwa ni Gabriel Endrew alimaarufu Dj BBG (43) mkazi wa Mwakibete jijini hapa.

 Amesema hilo  limetokea majira ya saa mbili asubuhi ambapo gari T161 CPP ilimgonga mtembea kwa miguu ambaye ni mtoto anayekadiriwa miaka 13 ambapo amefahamika kwa jina moja la Rechal na kumsababishia kifo wakati akikimbizwa hospitali.

Pia, aliongeza kuwa gari hiyo imekamatwa na dereva anashikiliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano na kwamba polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.




COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: GARI LA MBUNGE WA MBEYA MJINI (SUGU) LAGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO
GARI LA MBUNGE WA MBEYA MJINI (SUGU) LAGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhxUK8EH5YR1jNZDtkQRSaH_yZI-Pk8_jed61hMxj5IIV3m5fSjzYtLgazb3I75Dd84qyPZDw-wPSmIfYpU9_wbPNmHgMlFZljHGGSPj6HO6kDtbl2k6Px7CNFC06a9Sf4JXo6URhkjTsM/s640/sugu-mbunge.png
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhxUK8EH5YR1jNZDtkQRSaH_yZI-Pk8_jed61hMxj5IIV3m5fSjzYtLgazb3I75Dd84qyPZDw-wPSmIfYpU9_wbPNmHgMlFZljHGGSPj6HO6kDtbl2k6Px7CNFC06a9Sf4JXo6URhkjTsM/s72-c/sugu-mbunge.png
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/12/gari-la-mbunge-wa-mbeya-mjini-sugu.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/12/gari-la-mbunge-wa-mbeya-mjini-sugu.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy