CHUO KIKUU CHA ARDHI CHATOA ZAWADI KWA WANAFUNZI 104 WALIOFAULU
HomeJamii

CHUO KIKUU CHA ARDHI CHATOA ZAWADI KWA WANAFUNZI 104 WALIOFAULU

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Ardhi, Prof. Idrissa Mshoro (wa pili kulia) akiteta jambo na Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo ...

DIWANI KATA YA BUGURUNI MHE. ADAM AWAAGIZA VIONGOZI WA KUWAKAMATA NA KUWACHUKULIA HATUA WANANCHI WASIOFANYA USAFI.
RAIS MAGUFULI ATEUA MWENYEKITI WA BODI TTCL NA AWAAPISHA KAMISHNA JEN ANDENGENYE NA MABALOZI WANNE
BODI YA SHIRIKA LA POSTA YAWAPIGA CHINI VIONGOZI 2 WAANDAMIZI NA KUWASIMAMISHA 2




Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Ardhi, Prof. Idrissa Mshoro (wa pili kulia) akiteta jambo na Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho (Taaluma), Prof. Gabriel Kassenga(katikati kushoto), pembeni kulia ni Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa chuo hicho (Mipango, Fedha na Utawala),Prof. Robert Kiunsi, pembeni kushoto ni Maafisa Waandamizi wa chuo hicho. Shughuli hizo zimefanyika leo Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya chuo hicho.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi, Prof. Idrissa Mshoro akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa chuo na wanafunzi waliofanya vizuri kitaaluma wakati wa shughuli za ugawaji wa vyeti na zawadi kwa wanafunzi waliofaulu masomo mbalimbali uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya chuo hicho.
 
 
Mmoja kati ya washindi wa jumla wenye alama za juu, Lwijiso Anyighwile akipokea zawadi kutoka kwa mmoja wa wafadhili ambao ni Kampuni ya Hightech System mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi. Shughuli hizo zimefanyika leo Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya chuo hicho.
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
Chuo Kikuu cha Ardhi kimetoa zawadi na tuzo kwa wanafunzi 104 waliofanya vizuri kitaaluma ili kutoa hamasa kwa wanafunzi wengine kuweka juhudi katika masomo.
Zawadi hizo zimetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Idrissa Mshoro ambaye ametangaza kuwa jumla ya wanafunzi wanne kati ya waliofanya vizuri wamepata alama sawa hivyo kuibuka washindi wa jumla kwa mwaka 2016. 
Akisoma hotuba wakati wa sherehe hizo, Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho (Taaluma), Prof. Gabriel Kassenga amesema kuwa sherehe hizo zimekuwa zikiwezeshwa na wadau mbalimbali waliojitoa kwa hali na mali kutoa zawadi na tuzo kwa wanafunzi waliofaulu vizuri kwenye vipengele mbalimbali vya taaluma hivyo amewasihi wadau hao kuendelee kuunga mkono jitihada zinazofanywa na wanafunzi hao ili kuwashawishi wanafunzi wengine kufanya vizuri.
“Zawadi mbalimbali zinazotolewa na wafadhili zimekua zikiwasaidia wanafunzi hawa kuongeza tija kwenye maisha yao ya kielimu na kiuchumi kwani wengi wao wamekuwa wakizitumia fedha hizo kama mitaji ya kufanyia biashara pindi wamalizapo masomo yao,”alisema Prof. Kassenga.
Amefafanua kuwa mwaka huu umekuwa wa tofauti kwani idadi ya wanafunzi wanawake na wanaume waliopata tuzo hizo iko sawa tofauti na miaka mitatu iliyopita ambapo wanawake walikua wakiongoza kwa asilimia 3.7 kwa kupata tuzo nyingi wakati wanaume wakiwa ni asilimia 2.2. 
Prof. Kassenga ametaja baadhi ya zawadi zilizotolewa na wafadhili walioshiriki katika shughuli hiyo kuwa ni vyeti, Kompyuta mpakato (laptop),vifaa vinavyotumika katika kupimaji wa ardhi pamoja na fedha taslimu.Aidha, Prof. Kassenga ametoa rai kwa kwa wanafunzi wote waliomaliza chuoni hapo kuwa juhudi walizokuwa wakizionyesha wakati wa masomo waende wakaziendeleze katika jamii zinazowazunguka pamoja na kwenye shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa ili wakawe mfano bora kwa vizazi vijavyo.
Kwa upande wake Emily Elandogo ambaye ni mmoja kati ya wanafunzi waliopewa zawadi hizo amewashukuru walimu wa chuo hicho kwa elimu wanayoitoa ambayo itakua ni chanzo cha kuwaletea maendeleo sehemu yoyote watakapokuwa pia ametoa ushauri kwa wanafunzi wenzake kuitumia vizuri elimu waliyoipata ili iweze kuwasaidia katika maisha yao. 
Mahafali ya Kumi ya chuo hicho yanategemewa kufanyika Disemba 3 mwaka huu katika viwanja va chuo hicho ambapo wahitimu wa shahada mbalimbali watatunukiwa stahili pamoja na vyeti vyao. 
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: CHUO KIKUU CHA ARDHI CHATOA ZAWADI KWA WANAFUNZI 104 WALIOFAULU
CHUO KIKUU CHA ARDHI CHATOA ZAWADI KWA WANAFUNZI 104 WALIOFAULU
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhMO0TvRpS9e7mGMaUt0Drs7bKnUCFCu-zNnQWJY8ZHa2fI_kTvUW33r-tzqiI0TJe93wyf2s0KpAUW5ktC7nRm1pNaiQ0Hp_NjTDkMCD5SsPn3wDa2Jafj7z5vGbIO_wYeh8N3qVnAJFg/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhMO0TvRpS9e7mGMaUt0Drs7bKnUCFCu-zNnQWJY8ZHa2fI_kTvUW33r-tzqiI0TJe93wyf2s0KpAUW5ktC7nRm1pNaiQ0Hp_NjTDkMCD5SsPn3wDa2Jafj7z5vGbIO_wYeh8N3qVnAJFg/s72-c/1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/12/chuo-kikuu-cha-ardhi-chatoa-zawadi-kwa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/12/chuo-kikuu-cha-ardhi-chatoa-zawadi-kwa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy