Bi harusi mtarajiwa, Amina Mohamed akiwa katika pozi. Bi harusi mtarajiwa, Amina akiwa na uso wa furaha. Ni hivi ...
Bi harusi mtarajiwa, Amina Mohamed akiwa katika pozi.
Bi harusi mtarajiwa, Amina akiwa na uso wa furaha.
Ni hivi punde Bi harusi mtarajiwa, Amina Mohamed (wa tano kulia) atafunga Ndoa yake na mpendwa wake Ashrafu Issa, hapa akiwa katika picha ya pamoja wanafamilia.
Bi harusi mtarajiwa, Amina Mohamed akiingizwa katika ukumbini wakati wa shughuli yake ya kuagwa (kitchen mada) eneo la Sinza Mapambano Dar es Salaam ambapo leo 23 Dec 2016 baada ya Swala ya ijumaa anatarajia kufunga Ndoa na Mpendwa Mume wake katiaka maeneo hayo ya Sinza, mbele ni Muuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhumbili ambaye ni wifi wa biharusi mtarajiwa, Subira Mheta akiwa na furaha iliyopitiliza.
Bi harusi mtarajiwa, Amina Mohamed akitunzwa na mmoja wa mwanafamilia.
Kikundi cha akina mama wakitowa burudani kwa kupiga Dufu wakati wa hafla fupi ya kumuaga, Bi harusi mtarajiwa, Amina Mohamed iliyofanyika nyumbani kwao Sinza Mapambano Dar es Salaam.
Mmoja wa mwanafamilia akimtunza zuria la kufutia miguu.
Bi harusi mtarajiwa, Amina Mohamed katika pozi na Muuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhumbili ambaye ni wifi yake Bi harusi mtarajiwa, Subira Mheta. Bi Subira alipata nafasi ya kumuusia machache ili awe balozi katika familia. Ibada ilisisitizwa kuwa kipaumbele ili wadumu katika upendo na kuishi katika baraka za Allah.
Bi harusi Amina Mohamed akiondoka ukumbini tayari kwa kujiandaa na hafla ya Harusi yake itakayo fanyika leo baada ya Swala ya Ijumaa nyumbani kwao Sinza Mapambano Dar es Salaam.
Wana kikundi cha Upendo Group wakimtunza Bi harusi mtarajiwa, Amina Mohamed (katikati) ambapo ni wanakikundi wenzake na wifi yake, Subira Mheta. (Picha na Khamisi Mussa wa ujijirahaa blog)
COMMENTS