WAZIRI MWIGULU ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA NIDA JIJINI DAR ES SALAAM LEO
HomeJamii

WAZIRI MWIGULU ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA NIDA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kuma...

WATAKA SHERIA YA WATIA MIMBA WANAFUNZI IONGEZWE MENO
MSANIFU MKONGWE AACHA URITHI WA MAARIFA CHUO KIKUU ARDHI DAR ES SALAAM
WAZIRI MAKAMBA: MUUNGANO NI URITHI WETU, TU UTUNZE.





Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kumaliza kikao chake na Menejimenti ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya NIDA, Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo. Mwigulu aliwaambia waandishi wa habari kuwa, NIDA itaanza kutoa namba za utambulisho kwa wananchi wote kuanzia mwezi Desemba mwaka huu, ambao wamesajiliwa kupitia mpango wa usajili wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Andrew Massawe. (Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
 
 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Andrew Massawe (watano kushoto) akimuelezea jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati) wakati Waziri huyo alipotembelea Makao Makuu ya Mamlaka hiyo, Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo. Kiongozi huyo wa NIDA katika hotuba yake fupi kwa Waziri Mwigulu, alisema kuwa, NIDA itaanza kutoa namba za utambulisho kwa wananchi wote kuanzia mwezi Desemba mwaka huu, ambao wananchi hao wamesajiliwa kupitia mpango wa usajili wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). 
 
 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Mifumo ya Kompyuta (TEHAMA) wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Mohamed Khamis (wapili kushoto) alipokuwa akielezea jinsi wanavyosajili taarifa mbalimbali za waombaji wa vitambulisho. Waziri Mwigulu alitembelea Kituo hicho cha Usajili na kujifunza kazi mbalimbali zinazofanywa na NIDA, jijini Dar es Salaam leo. Watatu kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Andrew Massawe. 
 
 
 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Andrew Massawe (wapili kushoto-mbele) akimsindikiza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto mstari wa mbele) mara baada ya Waziri huyo kumaliza ziara yake ya kutembelea ofisi za NIDA Makao Makuu na ofisi zake za usajili wa taarifa mbalimbali za waombaji wa vitambulisho, zilizopo jijini Dar es Salaam.

……………………………………………………………..

Na Alex Mathias,Dar es salaam.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mh.Mwigulu Nchemba ametembela ofisi za Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na kukutana na uongozi mzima wa mamlaka hiyo na kusema kuwa ziara yake ni kwa ajili ya kuangalia suala nzima la uhakiki wa vitambulisho nchi Tanzania.


Akizungumza na waandishi katika makao makuu ya NIDA yaliyopo kinondoni mapema Leo jijini Dar es salaam Mh.Nchemba amesema kuwa ziara hii amekuwa akiifanya nchini kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na mamlaka hiyo kuja NIDA ni kwa ajili ya kuongea na uongozi kuhusu zoezi la uhakiki wa vitambulisho linavyoendelea.

“Nimetembelea sehemu mbalimbali nimekwenda katika mikoa mingi hapa Tanzania na jana nimetembelea zima moto pamoja na Magereza hata Mbeya nimefika pamoja na kuitembelea Timu ya Tanzania Prisons kwani nayo ipo chini yetu”alisema Nchemba

Aidha amesema kuwa baada ya kumalizika kwa zoezi la uhakiki wa vitambulisho NIDA itaanza kutoa namba za utambulisho kwa wananchi wote kuanzia mwezi Desemba mwaka huu, ambao wamesajiliwa kupitia mpango wa usajili wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Andrew Massawe amesema kuwa wanafurahi kutembelea na waziri Nchemba kwani ujio wake unaashiria kuwa tunafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na ukizingatia NIDA tumekuwa karibu na ofisi za uhamiaji.

“Kama alivyosema kuwa NIDA tumejipanga kuwa tutaanza kutoa namba za vitambulisho kwa wananchi wote na itaweza kuwasaidia hata katika kupanda magari ya mwendokasi hivyo ni jukumu letu kuhakikisha lengo letu linafika katika jamiii pamoja nanyi waandishi mmekuwa sehemu yetu kufikisha ama kuelimisha jamii kuhusu suala la kuhakiki vitambulisho”alisema Massawe

Hata hivyo amesema kuwa nia yetu ya kutaka kuanza kutumia namba ya vitambulisho ni kuondoa milolongo inayowakabiri wananchi wengi wanapoanza kutafuta vitambulisho mara nenda kule na itaweza kusaidia kuondoa utitiri wa vitambulisho ambavyo havina ubora au feki kwa watua wanaotumia.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI MWIGULU ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA NIDA JIJINI DAR ES SALAAM LEO
WAZIRI MWIGULU ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA NIDA JIJINI DAR ES SALAAM LEO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEixsT-LVWU-cW8mNemF8STyV89tUPycxDIiD6JZuIm07lfKo3sGpaGGwxiyF_1Cb4YbZjRfVoJbZx1yBLQKycoqu8bS-YjGg0yfx2_ltopVwr-KSeUkwHU23CdKBLbCv6pz2bc9smz1-QE/s640/NID1-768x510.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEixsT-LVWU-cW8mNemF8STyV89tUPycxDIiD6JZuIm07lfKo3sGpaGGwxiyF_1Cb4YbZjRfVoJbZx1yBLQKycoqu8bS-YjGg0yfx2_ltopVwr-KSeUkwHU23CdKBLbCv6pz2bc9smz1-QE/s72-c/NID1-768x510.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/11/waziri-mwigulu-atembelea-makao-makuu-ya.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/11/waziri-mwigulu-atembelea-makao-makuu-ya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy