WANANCHI WA MBAGALA-KIBURUGWA WAJADILI MAAGIZO YA RPC MUROTO KUHUSU ULINZI NA USALAMA
Kijana wa Mtaa wa Mbagala-Kiburugwa, Wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, akizungumza kwenye mkutano wa wakazi wa mtaa huo kujadili maagizo ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Temeke, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, (SACP), Gilles Muroto kuhusu masuala ya Ulinzi na Usalama kwenye ngazi ya Mtaa. Mkutano huo umefanyika
Novemba 20, 2016
HomeJamii

WANANCHI WA MBAGALA-KIBURUGWA WAJADILI MAAGIZO YA RPC MUROTO KUHUSU ULINZI NA USALAMA

Kijana wa Mtaa wa Mbagala-Kiburugwa, Wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, akizungumza kwenye mkutano wa wakazi wa mtaa huo kujadi...










Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Ulinzi na Usalama ya Mtaa wa Mbagala-Kiburugwa, Kassim Mohammed Mnyoge, akizungumzia maagizo hayo






NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
WAKAZI wa Mtaa wa Mbagala- Kiburugwa, wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, wamefanya kikao Jumapili Novemba 20, 2016, cha kujadili maagizo ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, (SACP), Gilles Muroto kuhusu masuala ya Ulinzi
na Usalama ngazi ya Mtaa.
Akizungumza kwenye kikao hicho, Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata Saleh Kaitani, alisema, kikao hicho kitajadili mambo mawili, mosi ni maagizo ya SACP Muroto na pili ni
masuala ya mpango wa kusaidia kaya masikini wa TASAF.
Kusuhusu suala la ulinzi na usalama, Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Ulinzi na Usalama ya Mtaa huo, Kassim Mohammed Mnyoge alisema, SACP Muroto katika kikao chake na
watendaji kilichofanyika Oktoba 28, 2016 kwenye shule ya msingi Kigungi, alitoa maagizo kadhaa kuhusu hatua za kuchukua katika kuhakikisha wananchi
wanashirikishwa katika suala la ulinzi na usala. “Kila mjumbe wa mtaa kwa kushirikiana na Mratibu, waorodheshe katika daftari wakazi wa mtaa husika ili kujua idadi yao na shughuli wanazofanya.” Alisema Bw. Kassim wakati
akiwasilisha taarifa kwa wananchi.

Mtaa wa Kiburugwa una wakazi wanaofikia 18,000 kwa mujibu wa Bw. Kassim.
Akifafanua zaidi kuhusu suala hilo la Ulinzi na Usalama, Bw. Kassim alisema, SACP Muroto ameagiza wananchi mjadili jinsi ya kushiriki katuika suala la ulinzi na usalama kwenye mitaa.
Kila mwenye nyumba, anapotembelewa na mgeni ni lazima akatoe taarifa kwa mjumbe wa nyumba kumi
au kwa mratibu wa eneo husika, lakini pia kila mwananchi lazima ashiriki kwenye suala la ulizni na akikaidi Mjumbe wa mtaa apelike taarifa kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa ili taarifa hiyo imfikia RPC kwa hatua za kisheria ambazo adhabu zake ni faini ya shilingi elfu 50,000 au kifungo cha miezi sita jela au vyote kwa pamoja. Maagizo mengine yaliyojadiliwa ni pamoja wazazi kuwadhibiti watoto wao, na endapo mtoto mwenye
umri chini   ya miaka 18 atajihusisha na vitendo vya
kihalifu kama kujiunga na makundi ya “panya road”, basi mzazi wa mtoto huyo atakamatwa kwa vile ni jukumu lake kuhakikisha mtoto huyo anakuwa katika maadili mema.

Wakichangia kwenye mjadala huo, wananchi wengi wamekubaliana na maagizo hayo ya kushiriki kwenye ulinzi lakini wakaonyesha wasiwasi namna ya utekelezaji wake.
“Ninapenda nijulishwe, ulinzi huu ambao wananchi tunatakiwa kushiriki ni wa namna gani, maana hali ya sasa sio kama ile ya zamani ya enzi za Mrema, mambo ya sungusungu
kutembea na panga nataka kujua tunalindaje na usalama wetu ukoje endapo nitadhurika.” Aliuliza mwananchi mmoja Bw.Hamisi Omary Libinongi.
Mwananchi mwingine, alisema, ni vema wananchi wanapolinda wakaongozana na askari wenye silaha, kwani wahalifu wa sasa, wanabeba silaha nzito nzito na kwamba itakuwa
hatari kwa mwananchi kufanya doria kwa kutumia panga pekee.
Akijibu hoja kuhusu jinsi ya ushiriki wa wananchi katika ulinzi, Mwneyekiti wa Serikali ya Mtaa huo, Bw.Said Mwinshehe Ng’agi, alisema, wananchi hawapaswi kuwa na wasiwasi katika suala hilo la ulinzi, kwani kila kundi la wananchi wanaolinda
kwenye eneo fulani, wataongozana na askari wawili wenye silaha.
Naye Kaimu Afisa
Mtendaji wa Kata hiyo ya Kiburugwa, Bw.Salehe Kaitani, amesema maagizo hayo ni ya serikali na wananchi hawana buni kushirikiana ili kuyatekeleza. “Wananchi tunapaswa kutekeleza maagizo haya ya Jeshi la polisi, najua zipo changamoto za
baadhi ya askari kutokuwa waaminifu, lakini kama mjuavyo askari wa namna hii ambao hawana wito, wamekuwa wakichukuliwa hatua na nyinyi wananchi toeni taarifa kwa viongozi kama mnakutana na askari wanaodai rushwa.” Alisema Bw. Laitani.






Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mbagala-Kiburugwa, wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mtaa huo, Said Mwinshehe Mng'agi, akiwa na Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata ya Kiburugwa, Salehe Kaitani, akifafanua baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wananchi
 Mwananchi akiuliza swali kuhusu utaratibu wa kiulinzi kwa kushirikiana na wajumbe wa mtaa.
  Mwananchi akiuliza nini umuhimu wa vijana wa ulinzi shirikishi kwenye mitaa.
 Mzee Hamisi Omary Libinongi, akkuliza namna wananchi watakavyotekeleza ulinzi huo bila ya kupatwa na madhara.
 Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata ya Kiburugwa, Salehe Kaitani, akifafanua baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wananchi.
 Mjumbe wa nyumba kumi, Bw. Jumanne Mohammed Ngayeka almaarufu kama "Nongwa" aliuliza swali.
  Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata ya Kiburugwa, Salehe Kaitani akihutubia wananchi.
 Wananchi wakifuatilia kwa makini kwenye mkutano huo.
 Mwenyekiti mstaafu wa serikali ya mtaa wa Mbagala-Kiburugwa, Mzee Adiswele, maarufu kama "Pepe Kale" akizungumzia uzoefu wake katika swala la ulinzi shirikishi.
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mbagala-Kiburugwa,
wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mtaa huo, Said Mwinshehe Mng'agi, (kulia) akizungumza na wananchi.

 Baadhi ya wananchi waliohudhuria
 Baadhi ya wananchi waliohudhuria







Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WANANCHI WA MBAGALA-KIBURUGWA WAJADILI MAAGIZO YA RPC MUROTO KUHUSU ULINZI NA USALAMA
WANANCHI WA MBAGALA-KIBURUGWA WAJADILI MAAGIZO YA RPC MUROTO KUHUSU ULINZI NA USALAMA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjqPvOmZlYvH0UrxeLvBfoGT_7ftCrQ_srsCDY4iX03jNKkZGlSVuJP1CMUhlveOUr1N2abDXpdgw65DTpeTo9QGzdidMY4DCjUjeqlpCSUSSWNcnlSO04ZECuQD8cqyEJoyvTIFXb9jpc/s640/5R5A3015.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjqPvOmZlYvH0UrxeLvBfoGT_7ftCrQ_srsCDY4iX03jNKkZGlSVuJP1CMUhlveOUr1N2abDXpdgw65DTpeTo9QGzdidMY4DCjUjeqlpCSUSSWNcnlSO04ZECuQD8cqyEJoyvTIFXb9jpc/s72-c/5R5A3015.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/11/wananchi-wa-mbagala-kiburugwa-wajadili.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/11/wananchi-wa-mbagala-kiburugwa-wajadili.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy