Serikali imesema itahakikisha inaimarisha uwezo wa kitaasisi ili kumudu vyema kazi za ufuatiliaji na tathmini ikiwa ni pamoja na...
Serikali
imesema itahakikisha inaimarisha uwezo wa kitaasisi ili kumudu vyema
kazi za ufuatiliaji na tathmini ikiwa ni pamoja na kutoa miongozo
mbalimbali itakayosaidia kuboresha utendaji kazi za Ufuatiliaji na
tathmini serikalini.
Hayo
yamesemwa leo na Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya
Utumishi wa Umma, Bi. Susan Mlawi alipokuwa akifungua Mafunzo ya siku
mbili ya Ufuatiliaji na Tathmini kwa Wizara mbalimbali yanayofanyika
Ofisi ya Rais-Utumishi.
Mlawi
alisema Mkakati wa Serikali wa kuimarisha Mfumo wa Ufuatiliaji na
Tathmini kwa taasisi hizo kunatonakana na kukosekana kwa mfumo madhubuti
wa Ufuatiliaji na Tathmini ambao ungetoa suluhisho la changamoto
mbalimbali zinazozikabili Taasisi za Umma nchini.
“Kukosekana
kwa mfumo madhubuti wa Ufuatiliaji na Tathmini katika taasisi za umma
nchini umesababisha kukwama kwa utekelezaji wa majukumu ya kila siku na
utoaji maamuzi sahihi,”
Bi.
Mlawi aliongeza. Alidha, Kaimu Katibu Mkuu huyo alizitaja baadhi ya
changamoto zinazoikabili Serikali kuwa ni pamoja na baadhi ya taasisi
zake kulalamikiwa na wananchi kwa kutoa huduma zisizoridhisha, utendaji
ambao haulingani na thamani halisi ya uwekezaji wa fedha za Umma katika
taasisi hizo, mchango mdogo wa baadhi ya Taasisi za Umma katika
kuchangia mapato katika Mfuko Mkuu wa Serikali, ongezeko la utegemezi
kwa Serikali kuu, uzalishaji na tija ndogo na ukosefu wa vipaumbele
katika taasisi hizo.
Akitoa
maelezo juu ya mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na
Ushauri wa Kazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba alitaja lengo
hasa la mafunzo hayo ni kubadilishana uzoefu katika
eneo la Ufuatiliaji na Tathmini ambayo washiriki wanayafanyia kazi,
kujenga uwezo wa Wataalam wa Ufuatiliaji na Tathmini kwenye Wizara zao
pamoja na kuona namna bora ya kuimarisha utendaji kazi katika taasisi za
Serikali.
“Eneo
la Ufuatiliaji na Tathmini limekuwa likilega leg asana katika taasisi
nyingi za Serikali hivyo tumeona ni vema tukakaa pamoja kuona namna bora
ya kuliimarisha,” Bw. Kiliba aliongeza.
Mafunzo
hayo yameanza leo na yanahudhuriwa na wajumbe kutoka Wizara 12 ambazo
ni Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Rais –Menejimenti ya utumishi wa Umma,
Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Ardhi, Nyumba na maendeleo ya
Makazi, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Wizara ya Maliasili na
Utalii, Wizara ya Katiba na Sheria na Tume ya Mipango.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora)
24 Novemba, 2016.
Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba akitoa maelezo kuhusu Mafunzo ya siku mbili ya Ufuatiliaji na Tathmini kwa Wizara mbalimbali yanayofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi Susan Mlawi, akifungua Mafunzo ya siku mbili ya Ufuatiliaji na Tathmini kwa Wizara mbalimbali yanayofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi.
Baadhi ya washiriki kutoka Wizara Mbalimbali wakifuatilia mada wakati wa Mafunzo ya Ufuatiliaji na Tathmini yanayofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi.
Mshiriki
wa Mafunzo ya Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Bi Mariam Silim akitoa neno la shukrani kwenye
Mafunzo ya Ufuatiliaji na Tathminiyanayofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi.
Mkurugenzi
Msaidizi, Sehemu ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji Kazi kutoka
Ofisi ya Rais - Utumishi, Bi Sakina Mwinyimkuu akiwasilisha mada kwenye
mafunzo ya Ufuatiliaji na Tathminiyanayofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi.
COMMENTS