Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda Sanga na msomaji wa taarifa ya pamoja ya Mtandao ...
- Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda Sanga na msomaji wa taarifa ya pamoja ya Mtandao wa wadau kutoka asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya sheria na sera ihusuyo usalama barabarani Tanzania akizungumza katika Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani inayoadhimishwa kila Novemba 20, 2016.
- Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda Sanga (katikati) na msomaji wa taarifa ya pamoja ya Mtandao wa wadau kutoka asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya sheria na sera ihusuyo usalama barabarani Tanzania akizungumza katika Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani inayoadhimishwa kila Novemba 20, 2016. Kulia ni Jones John kutoka Taasisi ya Jukwaa la Haki za Watoto Tanzania na Mwakilishi kutoka TAWLA, Nasieku Kisamby (kushoto).
- Taasisi ya Jukwaa la Haki za Watoto Tanzania, Jones John (katikati) akizungumza katika Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani inayoadhimishwa kila Novemba 20, 2016 iliyofanyika Ofisi za TAMWA jijini Dar es Salaam. Kulia ni Bi. Gladness Munuo kutoka TAMWA.
MTANDAO WA WADAU KUTOKA ASASI ZA KIRAIA UNAOTETEA MAREKEBISHO YA SHERIA NA SERA IHUSUYO USALAMA BARABARANI TANZANIA. SIKU YA KIMATAIFA KUWAKUMBUKA WAHANGA WA AJALI ZA BARABARANI 20 NOVEMBA, 2016.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Matukio
ya ajali za barabarani yamekuwa na athari nyingi hapa nchini kiuchumi
na kijamii. Vilevile matukio haya ya ajali za barabarani yamekuwa
yakiwasababishia wananchi madhara makubwa yakiwemo kupoteza maisha,
majeraha makubwa, ulemavu wa kudumu, mali kuharibika ikiwa ni pamoja na
kuacha familia nyingi zikiwa tegemezi baada ya kuondokewa na watu
wanaowategemea.
Takwimu
zinaonyesha kuwa takribani watu milioni 1.24 duniani hufariki kila
mwaka kutokana na ajali za barabarani, aidha, watu milioni 20 mpaka 50
hupata ulemavu. (Hii ni kutokana na takwimu za Shirika la Afya Duniani
(WHO). Kadhalika sehemu kubwa ya vifo na madhara ya ajali hizi
zimetokea Kusini mwa Jangwa la Sahara , Tanzania ikiwa moja ya nchi
hizo.
Takwimu
pia zinaonyesha kuwa ajali nyingi zinatokea kwa sababu ya makosa ya
kibinadamu hasa uzembe wa madereva kutokutii sheria na kanuni za
barabarani, ambapo kwa mujibu wa taarifa za jeshi la polisi nchini
Tanzania, asilimia 76% ya ajali barabarani husababishwa na uzembe wa
madereva, asilimia 8% husababishwa na ubovu wa barabara. Aidha ubovu wa
vyombo vya moto husababisha ajali kwa asilimia 16%.
Hata
hivyo ajali nyingi zinaepukika kama madereva na watumiaji wengine wa
barabara watazitii sheria na kanuni za Usalama barabarani.
Kutokana
na ajali hizo kuongezeka ndio maana ikatengwa siku maalum ya kimataifa
ya kuwakumbuka waathirika wa ajali za barabarani kila mwaka ambayo
huadhimishwa kila ifikapo tarehe 20 Novemba ya kila mwaka.
Siku
hii inatambulika kama siku rasmi ya kimataifa ya kuwakumbuka waathrika
wa ajali hizo na familia zao na kuzitaka nchi wanachama pamoja na
jumuiya za kimataifa kuitambua siku hiyo.
Pia
siku hiyo hutoa fursa kwa jamii nzima kukutana na kuwakumbuka wahanga
wa ajali za barabarani ,kutafakari madhara, gharama, na hatua zinazoweza
kuchukuliwa katika kuzuia ajali zisitokee. Vilevile siku ya kuwakumbuka
wahanga wa ajali za barabarani inatoa nafasi kwa wadau kuikumbusha
serikali wajibu wake na jamii nzima katika suala la kuzifanya barabara
kuwa sehemu salama kwa kila mmoja.
Hivyo
basi mtandao wa wadau kutoka asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya
sheria na sera ihusuyo usalama barabarani Tanzania kama ambavyo
unaratibiwa na Chama cha Wanawake Wanasheria (TAWLA) pamoja na mambo
mengine katika kuadhimisha siku hii tunaisihi serikali na watunga sheria
kuifanyia maboresho sheria ya Usalama barabarabi ya mwaka 1973 ili
iweze kukabiliana ipasavyo na suala la ajali za barabarani pamoja na
athari zinazotokana na ajali hizo
Maeneo ndani ya sheria ambayo mtandao huu utajielekeza kuona sheria inafanyiwa mabadiliko/maboresho ni pamoja na;
- Matumizi ya mikanda; Sheria ya sasa ya Usalama barabarani inasema ni kosa kisheria kwa dereva na abiria anayekaa kiti cha mbele kutokufunga mkanda wakati wa safari lakini sheria hiyo hiyo haisemi chochote kwa abiria wanaokaa kiti cha nyuma.
Utafiti
uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) unasema kuwa iwapo ajali
ikitokea madhara/athari kwa abiria wa kiti cha mbele itapungua kwa 50%
na kwa abiria wa nyuma madhara yatapungua kwa 70%. Kanuni zilizotungwa
na SUMATRA zinataka abiria wote wafunge mkanda ila kwa vile sheria mama
(Road Traffic Act of 1973) ipo kimya katika eneo hili utekelezaji wa
kanuni unakuwa mgumu.
Hivyo
basi ni rai yetu sheria hiyo ibadilishwe na kuwataka abiria wote
wanaokuwa katika chombo cha usafiri wa kibiashara au binafsi kufunga
mkanda wakati wote wa safari.
- Matumizi sahihi ya kofia ngumu; Sheria ya sasa ya usalama barabarani inasema kuwa ni kosa kwa muendesha pikipiki kutokuvaa kofia ngumu wakati wa kuendesha chombo hicho. Lakini sheria hiyohiyo haisemii chochote kwa abiria anayepanda katika chombo hicho.
Vilevile
pamoja na kuanishisha kosa kwa dereva wa pikipiki kutovaa kofia ngumu
lakini pia sheria haielezi ni jinsi gani kofia inatakiwa kuvaliwa na
aina maalum ya kofia inayotakiwa kuvaliwa.
Kwa
mujibu wa Utafiti wa Shirika la Afya Duniani (WHO) unaonyesha kuwa
iwapo ajali itatokea madhara yanayotokea kwa kutovaa kofia maalum na kwa
usahihi ni makubwa sana ukilinganisha na kofia hiyo ikivaliwa na kwa
usahihi. Hivyo basi ukizingatia kuwa sasa hivi usafiri wa pikipiki
umekuwa unatumika kwa kiasi kikubwa (public transport) hivyo ni rai yetu
sheria hiyo ifanyiwe maboresho na kuweka kuwa ni sheria kwa mtu yoyote
anayepanda pikipiki kuvaa kofia ngumu na kwa usahihi.
- Matumizi ya vilevi na uendeshaji vyombo vya usafiri: Sheria ya sasa ya usalama barabarani inasema kuwa itakuwa kosa kwa mtu yoyote kuendesha chombo cha moto akiwa na kiwango cha kilevi katika damu yake kinachozidi asilimia 0.08% katika mfumo wa mwili. Kiwango hiki ni kikubwa sana kikilinganishwa na tafiti zilizofanywa na Shirika la afya duniani na kupendekeza kiwango asilimia 0.05% kwa dereva aliyebobea (experienced driver) na asilimia 0.02% kwa dereva mchanga (young driver). Hivyo basi ni rai yetu kuwa sheria ifanyiwe marekebisho ili iendane na kiwango cha sasa cha kimataifa kilichofanyiwa utafiti.
- Mwendo kasi (Speeding): Mwendokasi umeendelea kuwa sababu kubwa ya ajali zinazogharimu uhai wa watu wengi. Sheria yetu inayo mapungufu kadhaa pamoja na juhudi nyingi za Jeshi la Polisi na wadau wengine kutaka kudhibiti jambo hili lemeendelea kuwa tatizo. Adhabu zisiszokidhi wala kuleta hofu kwa maderava wasiotaka kutii zimeendelea kufifisha juhudi za kudhibiti tatizo hili.
Tunatoa
wito kwa watunga sera kutaka kujihulisha zaidi na wadu kuuelimisha umma
zaidi katika eneo la uhusiano wa adhabu zitokanazo na makosa ya usalama
barabarani na ongezeko la ajali. Pia sheria kufanyiwa maboresho na
kuangalia kwa upya mianya iliyopo.
- Mwakilishi kutoka Chama cha wake Wanasheria Tanzania (TAWLA), Nasieku Kisamby (wa kwanza kushoto) akizungumza katika Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani inayoadhimishwa kila Novemba 20, 2016. Kutoka kulia ni Gladness Munuo, Jones John na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda Sanga.
- Ofisa Mradi Msaidizi kutoka Tanganyika Law Society (TLS), Mabhezya Rehani akizungumza katika Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani inayoadhimishwa kila Novemba 20, 2016.
- Meza kuu ikiwa imesimama kwa dakika mbili kuwakumbuka watu waliopoteza maisha kutokana na ajali katika Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani inayoadhimishwa kila Novemba 20, 2016.
- Christina Thomas mkazi wa Kibaha na mmoja wa waathiriwa wa ajali za barabarani akizungumza katika Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani inayoadhimishwa kila Novemba 20, 2016 iliyofanyika Ofisi za TAMWA jijini Dar es Salaam.
- Salum Juma Haji (kulia) makazi wa Buguruni jijini Dar es Salaam akizungumza jambo katika Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani inayoadhimishwa kila Novemba 20, 2016.
- Mkutano kati ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari pamoja ya Mtandao wa wadau kutoka asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya sheria na sera ihusuyo ukiendelea.
COMMENTS