Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Parole, Dkt. Augustine Mrema amemwandikia barua Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh...
Dkt.
Mrema ameyasema hayo mchana huu wakati wa kutoa taarifa yake hiyo kwa
waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam kuzungumzia suala lake hilo la
Maafisa wa Magereza kusitisha hatua ya kukatisha mpango wake licha ya
kuwalipia wafungwa waliokidhi vigezo.
“Mimi
nimeona nisinyamaze. Napaza sauti nataka Rais aone, ajue kama magereza
yetu yanashida na tunalotatizo kwa nini mpango huu umesimamishwa na
umesitishwa tumekosea wapi?.
Nimesha
muandikia barua Waziri Mkuu kulalamikia jeshi la Magereza kukwamisha
mpango huu na watu 43 tayari tumesha walipia faini hiyo lakini bado wapo
magerezani wanasota. Mrema amefanya kosa lipi? Ama Mama Mchungaji
Getrude Rwakatare amekosa nini? Mpaka wamesitisha zoezi hili” amesema
Mrema kwa waandishi wa habari.
Dkt.
Mrema ameweza kuonyesha nyaraka ikiwemo risiti mbalimbali walizofanya
malipo kwa ajili ya kuwatoa wafungwa hao ambapo amesema haki ya kuzuia
mpango huo imeweza kumuumiza vibaya kwani wasamalia wema walioweza
kujitolea fedha za mpango huo imewagusa pia.
Pia
ameongeza kuwa, mpaka sasa magereza mbalimbali kuna msongamano wa
wafungwa ambao wanahitaji msaada wa kutoka ila hawajapata fedha za
kulipiwa hivyo pindi wasamalia wema kama Mchungaji Mama Rwakatare
wanapojitokeza wanatakiwa kupongeza na wala si kupinda kona kona.Hivi
karibuni Jeshi la Magereza lilisitisha shughuli iliyokuwa ikiendeshwa
na Mchungaji Getrude Lwakatare ya kuwalipia faini wafungwa walioko
magerezani hadi hapo utaratibu mwingine utakapotolewa.
Awali
ilidaiwa kuwa Mpango huo unaofanywa na Lwakatare kwa kushirikiana na
Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Parole, Augustine Mrema tayari umewezesha
wafungwa 78 kutoka magerezani baada ya kuwalipia faini inayofikia Sh25
milioni.
Kwa
mujibu taarifa zilizonukuliwa katika moja ya vyombo vya habari hapa
mchini vilieleza kuwa, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Antonio Kilumbi
alisema amepata maelekezo ya kusitishwa kwa mpango huo kutoka ngazi ya
juu ya jeshi hilo na kuongeza kuwa, wananchi wengine bado wanaweza
kuwalipia faini hiyo ndugu zao.
Hata
hivyo Mrema alisema mpango huo ulilenga kupunguza msongamano
magerezani na kuipunguzia Serikali gharama za kuwahudumia wafungwa hivyo
kusitisha unarudisha nyuma juhudi za Bodi hiyo ya Parole katika
kuwasaidia wafungwa waliokizi vigezo
COMMENTS