Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea katika mkutano na waandishi wa habari akiwataarifu k...
Waziri
wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea katika mkutano na waandishi wa habari akiwataarifu kuhusu
kusomwa Bungeni kwa mara ya kwanza kwa Muswada wa Sheria ya Msaada wa
Kisheria wenye lengo la kuwa sheria yitakayosimamia na kuratibu utoaji
wa huduma ya msaada wa kisheria kwa watu wasio na uwezo wa kumudu
gharama za mawakili.
Mkurugenzi
Msaidizi Huduma za Kisheria kwa Umma Wizara ya Mambo ya Katiba na
Sheria, Felistas Mushi akiongea kwenye mkutano na Waandishi wa
habari kuhusu namna sheria ya Msaada wa Kisheria itakapopitishwa namna
itakavyofanya kazi na kuwasimamia watoa huduma za msaada wa kisheria.
Waziri
wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
akionyesha moja ya majarida yaliyotayarishwa na Sekretarieti ya Msaada
wa Kisheria katika kuelimisha Umma wakati Mratibu wa Sekretarieti hiyo
Bw. Daniel Lema (kushoto) akielezea juu ya upatikanaji wa msaada wa
kisheria hasa kupitia wasaidizi wa kisheria (paralegals). Mwingine
pichani ni Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Kisheria kwa Umma Wizara ya
Mambo ya Katiba na Sheria, Felistas Mushi.
Sehemu
ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo leo (23/11/2016)
katika ukumbi wa Mikutano Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria.
COMMENTS