MFUMUKO WA BEI WA TAIFA KWA MWEZI OKTOBA 2016, UMEBAKI KUWA ASILIMIA 4.5

Meneja wa Takwimu za Ajira na Bei wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ruth Minja, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaa...










Meneja wa Takwimu za Ajira na Bei wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ruth Minja, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa kuhusu mfumuko wa bei wa taifa wa mwezi Oktoba 2016. Kushoto ni Mtakwimu, Philbert Mrema.



 Mkutano na wanahabari ukiendelea.

 Wapiga picha wakichukua taarifa hiyo.

 Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kazini.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.


Na Dotto Mwaibale

MFUMUKO wa bei wa Taifa kwa mwezi Oktoba, 2016 umebaki kuwa ni asilimia 4.5 kama ilivyo mwezi Septemba 2016.

Hayo yamebainishwa na Meneja wa Takwimu za Ajira na Bei wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ruth Minja wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo.

"Hii inaamanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2016 imekuwa sawa na kasi ya upandaji wa bei ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba 2016" alisema Minja.

Minja alisema fahirisi za bei zimeongeza hadi 103.17 mwezi Oktoba, 2016 kutoka 98.72 mwezi Oktoba 2015 ambapo mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Oktoba 2016 umebaki kuwa asilimia 6.0 kama ilivyokuwa mwezi Septemba 2016.

Alisema mfumuko wa bei wa mwezi Oktoba umechangiwa na kuongezeka kwa kasi ya bei za bidhaa za vyakula na zisizi za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Oktoba 2016 zikilinganishwa na bei za mwezi Oktoba 2015.

Akizungumzia uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia shilingi 96 na senti 92 mwezi Oktoba 2016 ikilinganishwa na shilingi 97 na senti 04 ilivyokuwa mwezi Septemba 2015.

Aidha akizungumzia hali ya mfumuko wa bei kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki alisema nchini Kenya mfumuko wa bei wa mwezi Oktoba 2016 umeongezeka kidogo hadi asilimia 6.47 kutoka asilimia 6.34 mwezi Septemba 2016.

Alisema nchini Uganda mfumuko wa bei wa mwezi Oktoba 2016 umepungua hadi asilimia 4.1 kutoka asilimia 4.2 mwezi Septemba 2016.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MFUMUKO WA BEI WA TAIFA KWA MWEZI OKTOBA 2016, UMEBAKI KUWA ASILIMIA 4.5
MFUMUKO WA BEI WA TAIFA KWA MWEZI OKTOBA 2016, UMEBAKI KUWA ASILIMIA 4.5
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg9A-xKer0Er1iQEmYyZAUFspeoP_8Fm98jPp3GOgKLACqns0mLQQ6H8zuKwIHNdXukPqxy3zJpfZxhj9wpl0sa1R7qY0dJamfx18KnjyiHLXhpRtwbVxe_jGhp8c-LItLttNUoLGPnYgbW/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg9A-xKer0Er1iQEmYyZAUFspeoP_8Fm98jPp3GOgKLACqns0mLQQ6H8zuKwIHNdXukPqxy3zJpfZxhj9wpl0sa1R7qY0dJamfx18KnjyiHLXhpRtwbVxe_jGhp8c-LItLttNUoLGPnYgbW/s72-c/1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/11/mfumuko-wa-bei-wa-taifa-kwa-mwezi.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/11/mfumuko-wa-bei-wa-taifa-kwa-mwezi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy