Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inajipanga kuondoa utitiri wa kod...
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema
Serikali inajipanga kuondoa utitiri wa kodi mbalimbali zinatozwa kwenye
viwanda kama hatua ya kuviwezesha viwanda vingi nchini kuongeza
uzalishaji na kutoa ajira nyingi kwa watanzania.
Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo leo Jijini Arusha baada
ya kutembelea kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia cha Mount Meru
Millers ili kujua changamoto zinazokikabili kiwanda hicho ili Serikali
iweze kuzifanyia kazi katika kuleta unafuu kwenye uzalishaji wa mafuta
ya kupikia nchini.
Makamu
wa Rais amesema mlolongo wa kodi zinazotozwa kwa wamiliki wa viwanda
hazina uratibu mzuri hivyo mkakati ya Serikali wa awamu ya Tano inataka
kuweka utaratibu mzuri wa ulipaji wa kodi hizo ikiwemo kuondoa kodi
ambazo ni kero kwenye viwanda.
Amesisitiza
kuwa Serikali ya awamu ya Tano imedhamiria kuhakikisha viwanda vingi
vinajengwa nchini ambavyo vitatumia malighafi zinazozalishwa hapa nchini
hali ambayo itasaidia uuzaji wa bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi
kuuzwa kwenye masoko ya nje ya nchi na kuliingizia taifa mapato na
kuongeza ajira kwa makundi mbalimbali ya wananchi.
Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema ziara ambazo anafanya kwenye
viwanda mkoani Arusha ni kujionea jinsi viwanda hivyo vinavyofanya kazi
za uzalishaji na pale kwenye changamoto zinazokwamisha viwanda hivyo
kufanya kazi vizuri ziweze kufanyia kazi na Serikali.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mount Meru Millers Atul
Mittal amesema kama Serikali itafuta au kuondoa utitiri wa kodi
wanazotozwa kwenye Viwanda hivyo watakuwa na uwezo wa kuongeza maradufu
uzalishaji na kutoa ajira nyingi kwa Watanzania.
Amesema
kwa sasa Kampuni hiyo inafanya kazi kwenye nchi 10 barani Afrika na kwa
Tanzania pekee imeajiri wafanyakazi zaidi ya 1000 ambao wanafanyakazi
katika maeneo mbalimbali nchini.

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza na uongozi wa kiwanda cha Mt. Meru Millers mara baada ya
kufanya ziara kiwandani hapo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Makampuni ya Mt. Meru Bw. Atul Mittal akitoa taarifa kwa
Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan juu ya maendeleo ya kiwanda pamoja na changamoto wanazokutananazo
wafanyabiashara wazawa.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiangalia malighafi zinazotumika kuzalishia mafuta ya kupikia kutoka
kiwanda cha Mt. Meru Miller kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mt. Meru Bw. Atul Mittal akitoa ufafanuzi juu ya malighafi hizo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiangalia malighafi zinazotumika kuzalishia mafuta ya kupikia kutoka
kiwanda cha Mt. Meru Miller mjini Arusha.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akingalia ndoo za plastiki zinazotengenezwa na kampuni ya Mt. Meru
Millers kwa ajili ya kuhifadhia mafuta ya kula. Kulia ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Makampuni ya Mt. Meru Bw. Atul Mittal.





COMMENTS